Bolt Tanzania inasherehekea kuweka rekodi ya zaidi ya safari milioni 50 zilizohudumiwa kwenye mtandao wao, huku ikiwa kampuni ya usafiri mtandaoni inayoongoza barani Ulaya na Afrika kwa kusherehekea muongo mmoja wa huduma zake ulimwenguni. Pia imeshuhudia ongezeko la abiria mara 8 tangu ilipoanzisha uendeshaji wake sokoni.
Tangu kuzinduliwa kwake nchini Tanzania mwaka wa 2017, Bolt imetoa njia ya usafiri inayosifika zaidi, nafuu na yenye ufanisi, na kuunda fursa za ujasiriamali zilizopanuliwa na jumuishi zaidi zinazowezesha watu wengi zaidi kupata maisha endelevu. Bolt pia imeathiri vyema sekta ya uchukuzi nchini kwa kupunguza foleni ndani ya miji kwa kuhimiza chaguzi rahisi zaidi na za bei nafuu za usafirishaji.
Katika muongo mmoja uliopita, baada ya kuanza kama mwanzilishi wa kwanza, Bolt imebadilika na kuwa mtangulizi wa usafiri kimataifa, ulimwenguni kote na masoko ya ndani. Pia inasalia kulenga kutoa jukwaa la teknolojia bunifu ambalo linakuza usalama, uwezo wa kumudu na uendelevu.
Hivi karibuni, Bolt ilitangaza kuwa imepata wateja milioni 150 katika zaidi ya nchi 45 na miji 500. Wateja hawa wameenea katika kundi lake la bidhaa za usafiri ambazo ni pamoja na kukodisha gari, usafiri wa pikipiki (kukodisha bodaboda na bajaj), usafirishaji wa chakula, usafirishaji wa mboga, Bolt Drive, huduma ya kushirikisha safari kwa gari bila malipo, na Bolt Business, usafiri kwa makampuni. Bolt pia ilitangaza sasa kuna zaidi ya washirika milioni 3.5 (madereva na wasafirishaji mizigo) wanaotumia mtandao huo kujipatia riziki, wakiwemo zaidi ya milioni 1 barani Afrika pekee.
"Tunafuraha kuadhimisha hatua hizi muhimu katika kiwango cha kimataifa na cha ndani. Mafanikio haya ni ushahidi wa dhamira thabiti ya timu yetu ya kutoa bidhaa ya kipekee kwa waendeshaji wetu wanaothaminiwa na washirika wetu. Mtazamo wetu katika kutoa suluhu za kuaminika za usafiri umekuwa thabiti tunapotoa huduma kupitia magari ya kawaida, pikipiki na bajaji.
Lengo letu la kuhakikisha ubora, usalama, na ushirikiano ulioimarishwa wa madereva, hutumika kama msingi wa biashara yetu. Tunapoendelea kupanuka na kubadilika, tunaboresha nguzo hizi tatu mfululizo. Kwa mfano madereva sasa wanaweza kuwasiliana moja kwa moja na timu yetu ya ndani kupitia Kituo chetu cha Uhusiano wa Madereva jijini Dar es Salaam ambapo wanaweza kushughulikiwa masuala na hoja zao. Zaidi ya hayo, tunaendelea kushirikiana kikamilifu na vyombo vya udhibiti na washikadau ili kukuza mazingira ambayo yanakuza ukuaji wa sekta hii mahiri." Alisema Meneja Mkazi nchini, Charles Matondane.
Hatua kadhaa muhimu zilizofikiwa na Bolt Tanzania ni pamoja na:
● Imewezesha zaidi ya abiria milioni 50 kwa kuwaunganisha kwa urahisi na safari wanakoenda.
● Kuwezesha uchumi wa ndani na kukuza ujasiriamali kwa kuzalisha nafasi za kazi kwa zaidi ya madereva 10,000.
● Imeweka vitengo vya kisasa vya usalama na itifaki ili kuhakikisha ustawi wa abiria na madereva, kwa mfano, kitengo cha “Driver selfie” ambacho huimarisha usalama na pia huzuia uigaji wa madereva vishoka kushiriki kwenye akaunti.
● Ilizindua kituo chake cha kuwashirikisha madereva katika juhudi za kuimarisha uhusiano wa madereva na kushughulikia matatizo ya madereva katika kushughulikia zao.
Kwa mtazamo wa baadae, Bolt inabaki imara katika kuzingatia maadili yake ya msingi ya uwezo wa kumudu, usalama, kutegemewa, na ufikiaji.
Home
HABARI
Bolt Tanzania yaweka rekodi zaidi ya safari milioni 50 kwenye mtandao wake huku ikiadhimisha muongo mmoja wa shughuli zake kimataifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...