Raisa Said Korogwe

Chama  Cha Mapinduzi CCM mkoani Tanga kimenusa ubadhilifu wa fedha za Ujenzi wa majengo 14 za Hospitali ya wilaya Korogwe vijijini iliyogharimu Sh3.1 bilioni.

Hayo yamebaishwa Agost 11 na Mwenyekiti wa CCM mkoani hapo  Rajabu Abdurahman alipotembelea mradi huo unaotekelezwa na Serikali ambao unajengwa kwa awamu mbili.

Mradi huo utakapokamilika awamu ya pili utakuwa na majengo 22 ambapo gharama yake ni Sh7.5 bilioni.

Mwenyekiti wa chama hicho amesema fedha zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya Hospitali hiyo ya wilaya ya Korogwe vijijini  nia ilikuwa ni  kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu badala yake fedha zimedokolewa.

Rajabu amesema ipo miradi mingi ya kimaendeo fedha zake zimechezewa na CCM kitaandaa taarifa yake na kuipeleka makao makuu ya chama  kunielekeza Serikali hatua za kuchukua.

"Mradi huu wakati unaanza   najua ndugu zangu Mkuu wa Wilaya wa sasa Joket Mwegelo ,Mkurugenzi, Mganga Mkuu wa Wilaya na wegineo hamkuwepo lakini lazima tujifunze na haya yaliyofanywa na wenzetu kupitia mradi huu"amesema Rajabu

Alisisitiza kuwa  miradi mingine ambayo Rais Samia  ataleta fedha lazima muwe wakali na kuzisimamia fedha hizo za Serikali na zisichezewe na mtambue kuwa Chama na Serikali havijalala na hatua kali lazima zichukuliwe dhidi ya wabadhirifu hao.

Awali akisoma taarifa ya mradi huo Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt Miriam Cheche alisema kweli mradi huo ulikuwa na awamu bili ambapo awamu ya kwanza kutajengwa majengo 14 namengine yatajengwa awamu pili.

Alisema katika hatua hiyo ya awali walipokea Sh 1.8 billion kwa ajili ya majengo 7 ambapo majengo sita yalikamilika na yamekwishaanza kutumika tangu mwezi Juni 2020 isipokuwa jengo moja la utawala bado halijajengwa.

Dkt Cheche alieleza kuwa  katika awamu hiyo walipokea tena Sh 500 million kwa ajili ya majengo 3 ambapo hadi sasa limekamilika jengo moja tu la watoto na majengo mawili hayajakamilika.

Aidha alisema awamu ya tatu Serikali ilitoa tena Shs Mil 800 kwa ajili ya majengo 4 ambayo yapo katika hatua za mwisho ingawa zinahitajika zaidi Mil 160 ili kukamilisha majengo yote 14 ili kuweza kukamilisha mradi huo wa majengo 14 ya Hospitali hiyo ya Wilaya.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo alisema ujio wa Mwenyekiti huyo unakwenda kuwajenga,kuwasaidia na zaidi ya yote unakwenda kutoa muelekeo wa jinsi gani wanakwenda kuisimamia Serikali ambayo inaongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Korogwe Halfan Magani alisema ni kweli watumishi waliokuwa wanatekeleza mradi wa Hospitali hiyo ya Wilaya walitumia vibaya pesa za Serikali na hatua za kisheria zilichukuliwa dhidi yao.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...