Na Janeth Raphael - MichuziTv - Dodoma.
TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imefadhili miradi miwili wenye thamani ya Sh.milioni 120 kwa kila mradi kwa lengo la kufanya utafiti katika somo la hisabati kutokana na matokeo mabaya ya somo hilo katika mtihani wa darasa la saba na kidato cha nne.
Akizungumza leo Agosti 25,2023 na waandishi wa habari jijini Dodoma Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Tume hiyo Dkt.Amos Nungu amesema imeidhinisha miradi miwili kwa thamani ya Sh.milioni 120 kila mradi na utekelezaji wa mradi unahusisha watafiti kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini.
Amefafanua mradi utafanyika katika kipindi cha miaka miwili na hatua iliyopo sasa ni kusaini mikataba. "Somo la hisabati bado ni changamoto kwani matokeo yake yamekuwa mabaya kwa kidato cha nne na darasa la saba.
" Hivyo kwa kuondoa tatizo hilo Tume tumeidhinisha miradi miwili ambayo kila mmoja thamani yake ni Sh.milioni 120,"amesema na kuongeza miradi mingi ya utafiti hufadhiliwa kwa kipindi cha miaka miwili hadi mitatu.
"Kwa sasa ipo miradi kadha inayoendelea na ipo hatua mbalimbali ambayo Serikali ilifadhili kupitia COSTECH. Michache katika miradi hiyo ya utafiti inayoendelea katika hatua mbalimbali za utekelezaji, " amesema.
Ameongeza kwamba na Tume inafanya ufuatiliaji ikiwemo ile inayohusu kuboresha maabara za utafiti kwa ukarabati na ununuzi wa vifaa vya kisasa ikiwemo.
Pia amesema katika kuratibu, kukuza na kuendeleza utafiti, baadhi ya shughuli zilizotekelezwa ni pamoja na kuibua na kufadhili miradi ya kimkakati ambayo michakato imefanyika tayari na sasa ipo hatua ya mikataba ikiwemo kuyaelewa na kuyatumia vema mapinduzi ya nne ya Viwanda ndiyo mwelekeo kwa dunia nzima.
Dkt.Nungu amesema Serikali kupitia COSTECH imeidhinisha jumla ya miradi saba kwa thamani ya Sh.milioni 150 kila mradi. Miradi hiyo itafanyika ndani ya miaka miwili na inahusisha watafiti na wabunifu kutoka sekta zote umma na binafsi.
Amesema COSTECH inaendelea kuimarisha mfumo wa ubunifu nchini kwa kuanzisha au kutoa usaidizi kwa vituo mbalimbali vya ubunifu (intemediaries) ili kuwafikia na kuwahuduma wabunifu kiurahisi.
Pia kuweka mazingira wezeshi kwa ujumla wake katika ubunifu ni pamoja na kuwa na mfumo stahiki inayosaidia wabunifu na bunifu nchini."Tumekuwa na kumbi za ubunifu , kuwapokea na kuwalea wabunifu, Sera na miongozo, mitaji."
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia ( COSTECH) DKt Amos Mungu akizungumzia na wanahabari kuelezea utekelezaji wa majukumu yaliyofanyika ndani ya miaka miwili Katika Tume hiyo Leo Jijini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...