NA.VERO IGNATUS,ARUSHA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan,anatarajia kufungua Kikao Kazi cha wenyeviti wa Bodi na watendaji Wakuu wa Taasisi (CEOs)na Mashirika ya Umma ,kitakachofanyika Jijiji Arusha hapo august 19 katika Kituo cha Mikutano Arusha na kushirikisha jumla ya Taasisi 248 pamoja na wageni zaidi ya 1000

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi na Mkurugenzi wa Banki ya Biashara Tanzania Sabasaba Kitewita Moshingi amesema kikao hicho kimeandakiwa na Ofisi ya msajii wa Hazina, lengo kuu la kikao hicho kujadili muhimu kwa mustakabali wa nchi hususani katika suala nyeti la utendaji wa Taasisi za Umma.

Moshingi amesema kuwa kikao kazi hicho cha siku tatu ni kikao cha kwanza cha muda mrefu lengo likiwa ni kupokea kutoka kwa viongozi wa Kitaifa maono na mapendekezo yao kutoka kwa viongozi wa Taasisi za umma sambamba na kuwa na uzalishaji mzuri wenye kuzalisha faida na wenye tija kwa Taifa la Tanzania

''Tangu jana tumekuwa hapa kuandaa kikao hiki na kutakuwa na mada nyingi sana ambazo zitatolewa na watu mbalimbali waliobobea lengo likiwa ni kufanikisha na mambo mengi mazuri yatajadiliwa kwaajili ya manufaa ya nchi yetu,tutakuwa na Mhe.Waziri Mkuu,Spika wa Bunge la Tanzania,Katibu mkuu Kiongozi na baadhi ya Mawaziri,wenye viti pamoja na ma CEOs''.Alisema Moshingi

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amemshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ridhaa yake kuruhusu kikao hicho kufanyika Arusha,hivyo jambo hili kwa mkoa ni kubwa na kwa Taifa kwa ujumla kwani Taasisi hizi zina mchango mkubwa katika mfumo wa serikali katika kusimamia maendeleo ya nchi na watu.

Amesema Arusha ipo salama na wamejipanga na ni jukumu lao kuhakikisha ya kwamba mkoa mzima unakuwa salama na haswa maeneo ambayo washiriki wa mkutano watakuwepo kwa siku zote hizo,na amewaahidi kwamba watakuwa tayari wakati wote pale wnapohitajika kkuhakikisha kwamba mkutano unafikia malengo yaliyokusudiwa.

Aidha amewataka wana Arusha kuwa wakarimu kwa wageni pamoja na kulinda sifa ya mkoa,ambapo amewataka kwenye maeneo ya huduma wahakikishe kuwa zinakuwa za kiwango cha juu na pale wanapoweza kuboresha zaidi wafanye hivyo.

Awali akiwakaribisha wageni Mkurugenzi Mtendaji wa AICC Balozi Ephrahim Mafuru alisema kuwa AICC ni mjumbe wa Taasisi zinazo andaa mikutano mikubwa ya uchumi wa mikutano, ambapo kila mwaka wanapata taarifa za utendaji wa mikutano yote inayofanyika bara zima la Afrika,ambapo wanapima idadi na namba za washiriki pamoja na kuangalia ufanisi katika mikutano yenyewe.

Aidha Katika nchi zote za Afrika kwa mwaka 2019 katika mikutano zaidi ya 200 iliyofanyika Tanzania iliweza iliweza kuandaa mikutano 13 sawa na 5% ya mikutano yote iliyofanyika Afrika,hivyo mikutano yote iliyofanyika na huwa unarekodiwa kwajili ya kumbukumbu.

''Baada ya Mhe.Rais kuifungua nchi,haswa baada ya fiamu ya Royal tour ,na pia taasisi ya Aicc kuweza kufanya juhudi kubwa ya kujitangaza kimataifa mwaka 2022 katika mikutano yote iliyoandaliwa Tanzania imeandaa mikutano 18 sawa na 10% ya mikutano yote,Tanzania imeweza kutoka namba 11-5 ikiwa imetanguliwa na nchi zifuatazo Afrika ya kusini,Morrocco, Rwanda, Misri na Tanzania,ambapo tunaamini siku chache zijazo tutapanda hadi kuwa 3 bora hata zaidi''.Alisema Mafuru.

Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) ,Justina Mashiba amesema kuwa,mkutano huo ni wa kwanza kufanyika ambapo kamati ya maandalizi wapo tayari na kupitia mkutano huo kutakuwepo na mabadiliko makubwa mpya .

Amesema kuwa,mkutano huo utaanza agosti 19 hadi 21 ambapo mkutano huo unalenga kuleta mabadiliko mbalimbali ya teknolojia kupitia kwa wakuu hao wa Taasisi na wenyeviti kutoka mikoa mbalimbali.


Mwenyekiti wa jukwaa la viongozi wa Taasisi za Umma ,Sabasaba Kitewita Moshingi akizungumza na waandishi wa habari AICC Jijini Arusha.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania Tantrade Latifa.M.Khamis akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha mikutano cha kimataifa cha AICC,Ephraim Mafuru akizungumza katika kikao hicho na waandishi wa habari jijini Arusha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...