Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akifungua Kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma leo Jijini Arusha.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza na washiriki wa Kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma leo Jijini Arusha.
Katika picha ni baadhi ya Mawaziri walioshiriki Kikao kazi cha siku tatu cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma leo Jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki wa Kikao kazi cha siku tatu cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma leo August 19/2023 kinachoendelea Jijini Arusha.

Baadhi ya washiriki wa Kikao kazi cha siku tatu cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma leo August 19/2023 kinachoendelea Jijini Arusha.

 
NA. VERO IGNATUS, ARUSHA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ,amefungua Kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma leo Jijini Arusha ,huku akiweka wazi ujio wa maboresho ya Mashirika na Taasisi za Umma nchini.

Dkt Samia amesema upo umuhimu wa kuyaunganisha baadhi ya mashirika hayo huku akitoa onyo kwa watendaji na Mashirika na wenyeviti wa bodi, ambao watashindwa kutimiza wajibu wao kuwa watafikishwa katika vyombo vya sheria.

Aidha amesemama kuwa Mtendaji ambaye anaona hawezi kwendana na maboresho hayo ni bora amfate kumnong'oneza kubalishwa kazi,ambapo amewataka watendaji hao wasimlazimishe kufanyakazi wa kupangua nafasi kwani hapendi lakini ikibidi atapangua tu.

"Juzi niliwaapisha wakuu wa taasisi nilichowaasa ni kwamba nawakabidhi taasisi hizi,nendeni mkafanyekazi, ikifa na wewe ufie huko huko, usirudi kunisomea taarifa kushindwa kuzalisha, katika hili sitanii,maana serikali imewekeza fedha nyingi katika haya mashirika"alisema

Sambamba ma hayo Rais alisema kuwa Mchakato wa maboresho ya Mashirika na Taasisi za umma na wakala wa serikali unasimamiwa na ofisi wa msajili wa Hazina ambayo nayo itapandishwa hadhi na kufanywa mamlaka.

"Kuna mashirika ambayo yataunganishwa na mengine kuondolewa naagiza Ofisi ya hazina, kuzungumza na watendaji na mashirika hayo na kupata maoni yao kabla ya kuunganishwa ama kufutwa, kama wakiwashawishi kuwa wanaweza kuboresha utendaji kazi wao basi watazamwe"alisema

Alisema Tanzania kuna Mashirika na Taasisi 248 ambapo serikali imewekeza kiasi cha sh 73 trilioni, lakini bado mchango wa mashirika ni mdogo, ambapo huchangia asilimia 4, tu ya bajeti ya Taifa jambo ambalo halikubaliki.

Ameainisha changamoto za Mashirika hayo, ambapo ameiagiza Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji kufanya mabadiliko ya sera, huku akionya tabia ya baadhi ya watendaji serikali kwenda kuchukuwa fedha kwenye mashirika na kuyataka mashirika kuanza kujipanga kwa kuanza kuuza hisa zake..

"Tuache kuweka mikono kwenye mashirika, yaacheni yajiendeshe yenyewe yawe na tija kwa taifa na Serikali,.nakumbuka Nilipokuwa Waziri wa Maliasili Zanzibar, posho yangu ilikuwa kidogo lakini mwenzangu, alikuwa anafedha anachukuwa Tanapa, Ngorongoro na kwingine, anakuja na fedha nyingi, mimi nabaki kwenye Banda mwenzangu anazunguka madukani na kununua hiki na kile mimi nilikuwa nikibaki na kiposho changu cha chakula na hoteli"alisema

Sambamba na hayo Katika kikao hicho, Rais Samia Suluhu alikabidhi tuzo kwa baadhi ya mashirika ambayo yamefanyavizuri, ikiwepo kutoa gawio kubwa

Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu alisema Mashirika hayo ni Taasisi ambazo za kibiashara ambazo zimetoa mchango mkubwa ya kwanza ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzanioa (TCRA) ambao wamechangia kiasi cha Sh 272.4 bilioni wa pili Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), Sh 207.9 Bilioni huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa(NIDA)

Mashirika ambayo serikali ina hisa yaliyofanya vizuri ni Twiga Cement, wamechangia sh 84 bilioni, Benki ya NMB imechangia sh 45 bilioni na Kampuni ya simu ya Airtel ambayo serikali ina hisa imechangia sh 61 bilioni,

Kampuni nyingine ambazo zimefanya vizuri ni shirika la Madini la Taifa(STAMICO) na Shirika la Bima la Taifa(NIC) ambapo STAMICO miaka miwili iliyopita ilikuwa inategemewa kufutwa na mwaka huu wamechangia sh 2.2 bilioni 2.2 na NIC pia imefanya maboresho makubwa ya kuitendaji.

Makampuni ambayo yamefanya maboresho makubwa na kuongeza faida kuwa ni Shirika la Umeme(TANESCO) ambalo lilitengeneza faida ya bilioni Bilioni hukui Shirika la Nyumba Tanzania(NHC) nikipata faida ya sh 240 bilioni.

Mchechu alisema kuna mashirika ambayo yametoa gawio na yanamilikiwa na serikali kwa asilimia 100, ambapo ni shirika Maendeleo la Petroli ambalo limechangia sh 2.5 bilioni, Shirika la STAMICO sh 2.2 bilioni na shirika la bima la Taifa NIC sh 2 bilioni.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza katika kikao kazi hicho, alisema kumekuwepo na maboresho katika utendaji kazi katika mashirika ya umma, lakini pia bado kuna changamoto.

"Wito kwa watendaji wote wamashirika ya umma ni muhimu kuyazingatia yote ambayo Rais Samia Suluhu ambayo ataagiza na kuyaimarisha na yakatowe msingi wa kutoa msingi wa mwelekeo"alisema

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...