Na Janeth Raphael - MichuziTv - DODOMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhe. Angellah Kairuki amesema serikali itaendelea kufanyia kazi na kuweka mkazo wa kuwepo kwa mikutano ya kitaaluma ya waweka hazina na wahasibu ambayo itafanyika kila mwezi ili kuokoa upotevu wa mapato ya serikali.

Mhe. Kairuki ameyasema hayo leo Agosti 17,2023 Jijini Dodoma katika kikao kazi cha ukaguzi wa hesabu za mwisho wa mwaka wa fedha na waweka hazina na wahasibu wa sekretarieti za mikoa na mamlaka za mitaa ambapo amesema kumekuwa na changamoto kubwa hasa kwa maafisa wahidhiniwa na mawakala wanao kusanya mapato kwa niaba ya halmashauri.

"Wapo ombao wamepewa mashine za kukusanyia mapato lakini unakuta wengine unakuta wanazo mbili mbili, na yawezekana wengine tunawajua ni vyema tukafuatilia mienendo ya maafisa wetu wanao kusanya mapato katika vyanzo mbalimbali lakini vilevile utaratibu tunao utumia kuwapata mawakala wanao kusanya mapato katika halmashauri zetu, "amesema Mhe. Kairuki.

Aidha, ameongeza kuwepo kwa usimamizi mzuri wa mawakala wanaokusanya fedha kwa kuwa wengi wao hawapeleki makusanyo sehemu husika na muda maalum.

''Tuwe macho kwa wale wanaokusanya fedha na hawapeleki makusanyo yao sehemu husika ni vyema mkafanya usimamizi mzuri''Mhe.Kairuki

Pia ametaka wakaangalie tena vigezo wavyotumia kuwapata mawakala hao pale wanapohitajika pamoja na kuangalia historia zao katika masuala ya kifedha.

"Pengine unaweza kukuta niwezi hawana historia nzuri halafu hatujachunguza na tunakuja kuwapa madaraka makubwa ya kufanya kazi kwa niaba ya halmashauri, kwahiyo ni vyema nanyi mkaanza kufuatilia kuangalia kila chanzo,"amesema Mhe. Kairuki.

Amesema ni imani yake kuwa wataendelea kusimamia vyema vyanzo vya mapato na ukusanyaji wake na kuhakikisha wanapata mapato halisi na makubwa zaidi ikiwa ni pamoja na kusimamia vyema mfumo wa kazi ambapo kwasasa wanahudumia kuanzaia ngazi ya vijiji hadi kata.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Wahasibu ,Geogre Eston Mashauri amesema lengo la Mafunzo hayo ni kuangalia Tathimini ya hesabu zilizopita na kufanya mapitio ya ufungaji wa hesabu za mwaka huu ikiwemo kutatua changamoto zote ili kuhakikisha hakuna hoja inayoweza kujitokeza.

WAziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Angellah Kairuki akizungumza katika kikao cha ukaguzi wa hesabu za mwisho wa mwaka wa fedha na wahasibu pamoja na watunza fedha Leo Jijini Dodoma


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...