Na Mwandishi Wetu

CHUO cha Maendeleo ya Ujuzi, Ufundi na Viwanda (Furahika Education College) kilichopo Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam kimeendelea kuwafikia Watanzania walipo ndani na nje ya nchi kupitia maboresho mapya ya mfumo wao kujiunga na chuo bonyeza hapa

Akizungumza jijini Dar es Salaam Mkuu wa chuo hicho, David Msuya amesema Chuo cha Furahika Education College kwa sasa kimejipanga kukuwezesha wewe mwanafunzi kufanikiwa na kuongeza nguvu kazi katika jamii.

"Hapa Furahika tunatoa mafunzo darasani na kupitia mtandao, njia hii itakuwezesha kujifunza kutokea eneo lolote ulipo na utapata cheti chakoaada ya kuhitimu.Ni rahisi na popote."

Amefafanua chuo hicho ni kati ya taasisi chache za elimu nchini zinazounga mkono kwa vitendo juhudi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan za kuwapatia Watanzania elimu ujuzi ambayo imekuwa na matokeo chanya katika maisha yao.

Miongoni mwa masomo muhimu yatakayomuwezesha mwanafunzi kutimiza ndoto zake baada ya kuhitimu ni uchoraji wa ramani za nyumba ambapo wakufunzi wabobezi watamfundisha mwanafunzi namna ya kubobea eneo hilo lenye fursa lukuki nchini.

Pia amesema mwanafunzi atajifunza ufundi umeme kupitia wakufunzi mahiri waliopo katika Chuo hicho huku akifafanua mafunzo hayo yatakayomuwezesha kujifunza kuhusu ufundi umeme wa majumbani na umeme wa magari.

Kozi nyingine ni kompyuta ambapo wanafunzi watajiifunza programu mbalimbali na baada ya masomo watakuwa na uelewa wa kutosha kwa ajili ya kwenda kutumia maarifa hayo katika kuajiriwa au kujiajiri wenyewe.

Aidha chuo kinatoa mafunzo ya udereva wa magari na kila mwanafuzi atapata nafasi ya kujifunza udereva wa magari aina zote na vyombo mbalimbali vya moto.

"Ukiingia katika mfumo wa masomo online ya mwaka 2023/2024 utakutana na kozi za engineering wa majengo, human resource, cleaning and forwarding,hotel management, tourism and travel, computer ICT, computer application, kilimo na ufugaji, mafunzo ya huduma ndani ya ndege.

" Nyingine ni mapambo,ususi, make up,ushonaji umeme wa viwandan,ualimu wa chekechea, engineering na nyinginezo ambapo ni wnye ufaulu wa four kuanzia 30 na hata darasa la saba."






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...