MKUU wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camilius Wambura ametoa onyo kali kwa kundi la watu waliosambaza taarifa kwamba wanaandaa maandamano nchi nzima ili kuiangusha Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassani kabla ya mwaka 2025 .

IGP Wambura ametoa hilo leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu taarifa za kundi la watu kupanga maandamano hayo na kushawishi jumuiya ya Watanzania kuwaunga mkono na hoja zinazoendelea za mjadala wa mkataba wa Bandari unaoendelea.

"Sisi tuliamini suala la bandari linajibiwa kwa hoja na na vilevile tukaamini kwa sababu hawa watu walikwenda mahakamani wangeheshimu uamuzi wa mahakama lakini badala yake wametoka sasa na kuanza kutafuta ushawishi na kuwataka watanzania waingie kwenye maandamano ya nchi nzima.

" Na miongoni mwao mmoja amekwenda mbali zaidi na kueleza watahakikisha wanaangusha Serikali ya Jamuhuri ya muungano ya awamu ya sita, "amesema IGP Wambura

Hivyo amewataka wasitishe kabisa matamshi yao hayo ya kichochezi kwani watachukuliwa hatua kali za kisheria kwa uhaini wanaotaka kuufanya kwani yote ni makosa ya jinai kwani Jeshi la Polisi halitakaa kimya na kuwavumilia hiko wanachotaka kukifanya kuvunja amani iliyopo

" Kama mfikiria tuko kimya tuko kimya basi tutakwenda kuwaonyesha hatuko kimya kwa yeyote anayevunja sheria ya nchi hivyo niwatake watanzania wawapuuze watu hawa kwani Tanzania ni nchi ya amani na salama.

"Hawa wati waache na wasitake kuwashawishi na kuingiza nchi kwenye machafuko hatujawahi kufika huko na hatutofika kwenye machafuko, " amesema IGP Wambura.

Aidha Wachochezi hao wametakiwa kutambua kuwa Jeshi la polisi ni imara sana wasitikise kiberiti kama waliwahi miaka ya huko nyuma na wakaguswa wasithubutu kwenda hatua nyingine huko wanakoshawishi kwenda ni sehemu mbaya.

"Niwaombe wananchi muwe watulivu muendelee kuishi kwa amani mkiendelea kufanya shughuli zenu za kiuchumi kama ilivyokuwa desturi yenu."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...