Ujenzi wa kiwanda cha kisasa cha kutengeneza vioo kilichopo Kijiji cha Mkiu, Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa Pwani umefikia asilimia 90 ya ukamilishaji wake na tayari moja ya mtambo wake umewashwa kwa mara ya kwanza kujiandaa na uzalishaji wa bidhaa hiyo.

Mashine hizo zitatumia siku 21 ili kuwa tayari kuanza uzalishaji hatua ambayo inaashiria wakati muhimu katika mageuzi ya viwanda katika eneo hilo na kuleta madaliko makubwa kwenye sekta ya uzalishaji wa vioo nchini.

Kwa kuzingatia teknolojia ya kisasa na ubora wa bidhaa zitakazozalishwa, kiwanda hicho kinategemewa kuboresha uchumi wa nchi na kutoa fursa kubwa za ajira amabapo inakadiriwa Zaidi ya watu 7000 watapata ajira kwenye mradi huo.

 Mradi huu, ulioanzishwa mwaka jana, unatarajiwa kuanza uzalishaji mwezi Septemba mwaka huu, ukiahidi kuleta maongezeko  makubwa katika sekta mbalimbali.

Akizungumza wakati wa sherehe ya uzinduzi, Jack Feng, Mkurugenzi Mtendaji wa Sapphire Glass, alisisitiza umuhimu mkubwa wa mafanikio haya katika kuongeza akiba ya fedha za kigeni nchini Tanzania.

Pia alisema  kuwa tukio hilo ni hatua kubwa katika utengenezaji wa kioo ndani ya Tanzania na eneo lote la Afrika Mashariki na Kati

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Prof. Kitila Mkumbo wakati wa ziara yake wiki mbili zilizopita aliipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji jambo ambalo limevutia mitaji mikubwa ya uwekezaji katika eneo la Afrika Mashariki na Kati.

Moja ya faida kubwa kwa nchi ni asilimia 80 ya malighafi zitakazo tumika katika kiwanda hicho zitatoka ndani ya nchi na kupunguza gharama za uzalishaji wa kiwanda hicho. ‘’Sapphire Float Glass (Tanzania) Limited, inaleta faida nyingi za kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kupunguza matumizi ya uagizaji wa bidhaa za vioo kutoka nje ya Tanzania, kuongezeka kwa mapato ya fedha za kigeni na kupanua mauzo kufikia nchi jirani’’ alisema Prof. Mkumbo.Baada ya kukamilika, mradi utakuwa na uwezo mkubwa wa uzalishaji unaokadiriwa kuwa tani 500 -700 za vioo kwa siku.

 Uwezo huu wa uzalishaji unatarajiwa kukidhi na kuzidi mahitaji ya vioo nchini Tanzania na nchi za Afrika Mashariki na katiMbali na vioo vya ujenzi, Kampuni ya Sapphire Glass Company Limited inakusudia  kuzalisha bidhaa mbalimbali za vioo, ikiwa ni pamoja na chupa za vioo, kikombe, vioo vya magari, na bidhaa nyingine za vioo zinazohusiana.

Mbali na mapato ya ndani, kiwanda hicho kitakua na Uwezo wa kuvutia mauzo ya nje ya bidhaa unaotarajiwa kufikia dola milioni 75 kwa mwaka, ambapo asilimia 70-80 ya bidhaa zitaelekezwa kwa masoko ya kimataifa.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...