
Na Mwandishiwetu, Michuzi TV
Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete na makamu mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm, Abdurahman Kinana wamemuandikia barua mhariri wa gazeti la Mwanahalisi, Said Kubenea wakimtaka kuomba radhi dhidi ya taarifa iliyochapwa na gazeti hilo Julay 20, 2023.
taarifa hiyo iliyochapishwa inadai, viongozi hao ( Kikwete na Kinana) wanalipa fedha watu wanaopinga mkataba wa uwekezaji kati ya serikali na kampuni ya dp world ya dubai.
Barua ya viongozi hao hiyo iliyoandikwa na kampuni ya wakili Eric s. Ng’maryo inamtaka mhariri wa Gazeti hilo Said Kubenea kufuta kashfa dhidi ya viongozi hao na kuomba radhi ndani ya siku 14, la sivyo watachukua hatua za kisheria.
Barua hiyo ya madai imeeleza kiini cha kashfa hiyo ni tuhuma za uongo kwamba viongozi hawa wanachochea wale wanaopinga maendelezo ya bandari kwa kuwalipa fedha watu ambao hawajatajwa ili watu hao wapinge au waendelee kupinga maendelelezo ya bandari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...