Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP Mzee Ramadhani Nyamka ametembelewa na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Shia, Sheikh Hemed Jalala nyumbani kwake leo Agosti 27, 2023 Goba, jijini Dar es Salaam. Pichani Kamishna Jenerali wa Magereza Mzee Ramadhani Nyamka(kulia) akikabidhiwa vitabu vya Dini na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Shia, Sheikh Hemed Jalala (kushoto) kwa ajili ya wafungwa na mahabusu waliopo Magerezani.
Kamishna Jenerali wa Magereza, Mzee Ramadhani Nyamka(wa pili kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Sheikh Mkuu wa Madhehebu ya Shia nchini, Sheikh Jalala (wa kwanza kushoto) na ujumbe wake leo asubuhi walipokutana na kufanya mazungumzo yenye lengo la kufahamiana na kuona namna ambavyo wanaweza kushiriki katika Urekebishaji wa wahalifu kupitia huduma za Dini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...