Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
Agost 12

Changamoto kubwa ya ukosefu wa huduma za kiafya iliyokuwa ikiwakabili wakazi wa mitaa ya Saeni,Zogowale na Jonung"ha ,kata ya Misugusugu,Kibaha Mkoani Pwani,imebaki historia baada ya ujenzi wa mradi wa Zahanati ya Saeni kukamilika.

Changamoto hiyo ilikuwa maumivu na kero kwa wakazi hao ambapo ilisababisha baadhi ya wajawazito kuzalia njiani na wengine kukosa huduma za haraka kwa kufuata huduma Mlandizi ambako ni mbali.

Akizindua Zahanati hiyo,Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka alieleza kukamilika kwa mradi huo ni kutimiza kwa ahadi ya CCM waliyotoa 2016-2017 wakati wa uchaguzi.

Alieleza, wakati wanafika eneo la Misugusugu alipokea kero kubwa tatu ikiwemo ukosefu wa Zahanati, barabara na maji machafu ambayo yalikuwa hayafai kwa afya ya binadamu.

"Nina furaha ya kipekee, kwasasa kero zote kupitia Diwani, Mbunge na Serikali Kuu ya Rais Samia Suluhu Hassan imeweza kutimiza ahadi hizo Misugusugu ,na Sasa Kuna Zahanati,maji safi na barabara" Kabla ya kuanza mradi huu mimi niliweza kuchangia milioni 6.5 ili kuunga mkono juhudi za wananchi kuanza ujenzi "alifafanua Koka.

Alieleza, Halmashauri imechangia million 75, Serikali Kuu milioni 100 na Mbunge milioni 6.5.

Koka alibainisha lengo lake kubwa ni kuwatumikia wananchi wake hivyo atahakikisha kuwa ataendelea kuboresha zaidi huduma ya afya ili wananchi waweze kuondokana na kero ambazo wamekuwa wakizipata.

Awali Mganga Mfawidhi wa Halmashauri ya Mji Kibaha,Dkt. Peter Nsanya alieleza ujenzi huo umegharimu sh.milioni 181.

Alieleza, Zahanati hiyo ina madawa,vifaa tiba na Sasa wanatarajia kutatua changamoto ya samani.

Vilevile, Diwani wa Kata ya Misugusugu Upendo Ngonyani alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini kwa kusimamia utekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi,ila anasema,bado inatakiwa milioni 7.1 kwa ajili ya samani ikiwemo viti,meza .

Ngonyani alieleza, Zahanati hiyo ni mkombozi kwa wakazi wa Misugusugu.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha,Mussa Ndomba alikemea tabia ya watu wachache kukwamisha juhudi za Serikali pamoja na Mbunge kuleta maendeleo Jimbo la Kibaha Mjini.

Alieleza, Serikali inafanya makubwa , inaelekeza fedha nyingi kukamilisha miradi, mbunge anasimamia ipasavyo hivyo waachwe wafanye kazi.

Ndomba aliwataka wanachama wa CCM na viongozi waendelee kuisemea Serikali kwa mazuri inayoendelea kufanya na kuwaeleza wachache ambao hawaoni yanayofanyika.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...