Na Mwandishi wetu Dodoma
MTENDAJI Mkuu Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) Mhandisi Seff Victor amesema hadi Mwezi Machi, 2023 TARURA imejenga madaraja 163 ya mawe yenye thamani ya Shilingi bilioni 8.7 ambapo gharama imepungua kwa zaidi ya asilimia 50 kwa kutumia malighafi zinazopatikana maeneo ya kazi ili kupata ufanisi wa gharama za ujenzi.
Haya ameyasema leo jijini hapa na Mtendaji huyo wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji na viapaumbele vya bajeti ya a mwakawa wa Fedha 2023/24.
Mtendaji huyo amesema Madaraja hayo yamejengwa katika mikoa ya Kigoma 92, Singida 24, Tabora 5, Kilimanjaro 10, Mbeya 2, Arusha 6, Mrorgoro 2, Rukwa 3, Pwani 1, Ruvuma 3 na Iringa 15 .
Pia Amesema wanaendelea kufanya majaribio ya tekinolojia mbalimbali ili kutumia udongo uliopo eneo la kazi badala ya kusomba kutoka maeneo mengine ya mbali..
"Tekinologia hizo ni pamoja na ECOROADS, Ecozyme, na GeoPolymer
Lakini pia kipaumbele cha TARURA ni kutumia malighafi zinazopatikana maeneo ya kazi ili kupata ufanisi wa gharama za ujenzi," Amesema Mtendaji huyo Victor .
Na kuongeza "Hadi sasa kwa kutumia Teknologia ya ECOROADS Katika Jiji la Dodoma imejengwa km 1 ambayo imekamilika na Katika Wilaya ya Mufindi zitajengwa km 10 na Mkandarasi yuko kwenye matayarisho ya kuanza kazi," Amesema .
Katika mwaka wa fedha 2023/24
Amesema jumla ya Barabara zenye km 21,057.06 zitafanyiwa matengenezo, km 427 zitajengwa kwa kiwango cha lami, km 8,775.62 zitajengwa kwa kiwango cha changarawe, madaraja na makalavati 855 yatajengwa na mifereji ya mvua km 70.
Ameeleza Jumla ya Shilingi bilioni 858.517 zimeidhinishwa kwa ajili ya Ujenzi, Ukarabati na Matengenezo ya Miundombinu ya barabara za Wilaya ambapo Kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 710.31 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 148.207 ni fedha za nje kupitia miradi ya RISE, TACTIC, Bonde la mto Msimbazi na Mradi wa Agri connect.
Aidha, Wakala umekwisha tangaza kazi za ujenzi na matengenezo ya miundombinu ya Barabara zaidi ya asilimia 60 ya mpango wa mwaka 2023/24 ambapo baadhi ya kazi utekelezaji umeanza.
Mtendaji Mkuu wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) Mhandisi Seif Victor akiongea na wanahabari kuelezea utekelezaji na vipaumbele ya TARURA kwa mwaka 2023/2024
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...