Na Shalua Mpanda,TMC Habari

BARAZA la Madiwani manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam limekaa kikao chake cha robo ya nne ya mwaka 2022/2023 ambapo pamoja na mambo mengine limepokea taarifa mbalimbali kutoka kwenye kata 23 za Wilaya hiyo

Kikao cha baraza hilo kimeongozwa na Mwenyekiti wake Meya wa Manispaa ya Temeke Abdallah Mtinika ambapo pamoja na mambo mengine kimejadili taarifa hizo sambamba na kuulizwa maswali na kupata majibu.

Kutokana na umuhimu wa kikao cha baraza hilo watendaji kutoka Kata zote 23 za manispaa hiyo wameshiriki na wameweza pia kujadili muhtasari mbalimbali ya vikao vilivyopita vya halmashauri hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya Meya mara baada kikao hicho, Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke Arnold Peter amesema halmashauri hiyo imejipanga kuhakikisha inamalizia ujenzi wa shule za sekondari katika kata tatu zilizobaki ili kukamilisha ujenzi wa shule hizo katika kata zote.

"Tumekuwa na kikao kizuri leo kikiongozwa na Meya pamoja na Mkurugenzi wa Manispaa,wananchi watarajie mambo mazuri, " amesema Arnold.

Awali wakati wa kipindi cha maswali na majibu, Siwani wa Viti Maalum Zame Mwadunia alitaka kujua ni lini halmashauri itakamilisha ahadi yake ya kukarabati masoko ndani ya wilaya hiyo.

Ambapo Mkurugenzi wa Manispaa Elihuruma Mabelya wakati anajibu swali hilo amelihakikishia baraza hilo kuwa tayari mhandisi wa Manispaa ameanza kazi ya upembuzi yakinifu ili kuanza ujenzi huo.

Kuhusu baraza hilo la madiwani ni kwamba kwa mujibu wa ratiba hukaa vikao vyake vilivyopo kisheria kila mwaka pamoja na vikao vingine vya Kamati,hukaa vikao vinne katika mwaka kupokea za kiutendaji kutoka kila kata ambapo kikao hiki ni cha robo ya mwisho cha mwaka 2022/2023.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...