Na.Mwandishi Wetu,Dodoma


Matumizi ya Teknolojia mbadala na malighafi zinazopatikana maeneo ya kazi kwa ajili ya ujenzi wa barabara na madaraja imeweza kupunguza gharama zaidi ya 50%.

Hayo yameelezwa Jana na Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Maelezo jijini Dodoma.

“TARURA imeweka kipaumbele cha kutumia malighafi zinazopatikana maeneo ya kazi ili kupata ufanisi wa gharama za ujenzi.

Mhandisi Seff amesema hadi kufikia mwezi Machi,2023 TARURA imejenga madaraja 163 ya mawe yenye thamani ya bilioni 8.7 ambapo gharama imepungua.

Ametaja mikoa iliyojengwa madaraja hayo ni Kigoma (92),Singida (24), Tabora (5), Kilimanjaro (10), Mbeya(2), Arusha (6), Morogoro (2), Rukwa(3), Pwani (1), Ruvuma (3) pamoja na Iringa (15).

Aidha, amesema bado wanaendelea kufanya majaribio ya teknolojia mbalimbali ili kutumia udongo uliopo eneo la kazi badala ya kusomba kutoka maeneo mengine ya mbali.

“Teknolojia hizo ni pamoja na Ecoroads, Ecozyme na GeoPolymer ambao hadi Sasa kwa kutumia teknolojia ya Ecoroads katika jiji la Dodoma imejengwa Kilomita moja(1) ambayo imekamilika na katika Wilaya ya Mufindi zitajengwa Kilomita kumi(10)”Aliongeza.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...