MSANII maarufu nchini Mrisho Mpoto a.k.a Mjomba pamoja na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Bongo Star Search Rita Paulsen 'Madame Rita' wameteuliwa kuwa mabalozi wa Baraza la Sanaa Tanzania( BASATA).
Akizungumza leo Agosti 15, 2023 jijini Dar es Salaam Katibu Mtendaji wa BASATA Dk.Mapana amesema wanatambulisha Mpoto kuwa Msemaji na Balozi wa baraza hilo pamoja na Madame Rita ambaye pia ameteuliwa kuwa balozi wao.
Kwa upande wake Mrisho Mpoto amesema amepokea kwa furaha kubwa uteuzi huo na kwamba sasa wakati umefika wasanii walioko pembezoni kupata jukwaa la kuonesa kazi zao.
Amesisitiza kuimarisha maadili na uadilifu pamoja na kutoa elimu kwa wasanii wenzake kuheshimu sheria za nchi pamoja kufanya kazi zenye maadili na zenye maslahi mapana kwa Taifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...