*Mikoa 26 kukusanywa kazi za Filamu *

     Na.Khadija Seif, Michuziblog
 
BODI  ya Filamu nchini yafungua rasmi dirisha la kuwasilisha na kukusanywa kwa kazi za Filamu kwa Mikoa 26 msimu wa tatu wa tuzo za Filamu ambapo Kilele chake kinatarajiwa kuwa  Disemba 16,2023.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt.Kiagho Kilonzo amesema tuzo za Filamu zimeimarika na kuwa na maboresha katika vipengele mbalimbali ikiwemo kipengele cha hadithi ndefu ambapo kwa misimu miwili iliyopita kipengele hicho hakikuwepo.

" wote tuna tambua tuzo hizi zipo kwa lengo la kuwapa moyo wasanii wetu wa Filamu katika kazi zao pamoja na  kuongeza chachu na ushindani kuzalisha kazi zenye ubora wa Kimataifa zenye stori za kufundisha jamii zetu."

Aidha  Kilonzo ameongeza kuwa kwa tuzo za Filamu 2023 limefanya mabadiliko na ongezeko la Mikoa 26 itakakusanywa kazi  mwaka huu badala ya mwaka jana mikoa 25 ilikusanya kazi.


"Zoezi la kupokelewa likitamatika lifata zoezi la Majaji kufanya mchujo na kazi zitazopita zitapata nafasi ya kuonyeshwa katika luninga ambapo tumezoea kuona azam tv ila kwa mwaka huu tumetoa nafasi kwa wadau wengi kupata nafasi hiyo ya kuzionyesha".

Aidha,Kilonzo amesema zoezi la kukusanywa litadumu kwa wiki 6 kuanza Agosti hadi septemba 25,2023 ambapo filamu zitapokelewa kwa njia 3 ikiwemo Msanii kuleta kazi katika Ofisi ya bodi ya filamu Kivukoni Jijini Dar es salaam,njia ya tovuti pamoja na kamati ya tuzo kufika kila Mkoa husika kuzikusanya.

Nae Mkongwe wa tasnia ya Filamu nchini Ahmed Olotu maarufu Mzee Chilo amewapongeza bodi ya filamu kwa kuendelea kuthamini kazi za wasanii na kuwapa motisha kwa wasanii kutengeneza kazi zenye ubora na za kishindani.

Pia amesema wasanii wakongwe wasisite kushiriki kikamilifu tuzo hizo kwani mbali na tuzo wasanii wamekuwa wakipata fursa ya kutembelea vivutio vya utalii vya Mkoa husika.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...