Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb), akifungua kwa niaba ya Spika wa Bunge Mkutano wa vikao vya Jukwaa la Kibunge la Nchi za Maziwa Makuu (Forum of Parliaments of the Great Lakes Region- FP-ICGLR) katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam. 

Kamati za Jukwaa hilo zinazotarajiwa kufanya vikao kwa nyakati tofauti ni Kamati ya Ulinzi na Usalama na Kamati ya Demokrasia na Utawala Bora.Wabunge wa Bunge la Tanzania ambao ni Wajumbe wa Jukwaa hilo pamoja na Wajumbe wengine kutoka Mabunge ya Nchi takribani 12 za Maziwa Makuu wanatarajiwa kushiriki katika vikao hivyo.

Katibu Mkuu wa Jukwaa la Kibunge la Nchi za Maziwa Makuu (Forum of Parliaments of the Great Lakes Region- FP-ICGLR), Balozi Onyango Kakoba akizumgumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa vikao vya Jukwaa la Kibunge la Nchi za Maziwa Makuu (Forum of Parliaments of the Great Lakes Region- FP-ICGLR) Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Wabunge wa Bunge la Tanzania ambao ni Wajumbe wa Jukwaa la Kibunge la Nchi za Maziwa Makuu (Forum of Parliaments of the Great Lakes Region- FP-ICGLR), Mhe. Eng. Ezra Chiwelesa (kushoto), Mhe. Dkt. Christine Ishengoma (katikati) na Mheshimiwa Deus Sangu (kulia) wakimsikiliza Naibu wa Spika Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb), akifungua Mkutano wa Vikao vya Jukwaa hilo  Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Wabunge wa Bunge la Tanzania ambao ni Wajumbe wa Jukwaa la Kibunge la Nchi za Maziwa Makuu (Forum of Parliaments of the Great Lakes Region- FP-ICGLR), Mhe. Najma Giga (kushoto) na Mhe. Shamsia Mtamba (kulia) wakimsikiliza Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb), akifungua Mkutano wa Vikao vya Jukwaa hilo  Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.

PICHA NA BUNGE

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...