Na.Khadija Seif,Michuziblog
WASANII na wadau wa tasnia ya Muziki nchini waaswa kuzikimbilia fursa za Kimataifa zilizopo kwenye Muziki ili kuongeza walaji na kutangaza kazi zao Kimataifa kupitia mifumo ya kupakua kazi hizo duniani kote.
Akitoa wito huo Leo Agosti 15,2023 wakati akizungumza na Wanahabari Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Dkt.Kedmon Mapana wakati wa kuzindua Mkutano wa Muziki barani Afrika amesema Mkutano huo ni kwa mara ya pili unaenda kufanyika nchini Tanzania ni fursa kwa Wizara na taasisi zake kwa ujumla kuona kwa namna gani bahati hii imerudi kwa mara nyingine lengo hasa ni kuwapa kipaumbele wasanii wakitanzania zaidi kujifunza vingi kupitia muziki wao.
"Mkutano huu wa Access Music sio tu kuwapatia fursa wasanii kujifunza vitu mbalimbali pia inawapa nafasi wadau kutangaza kazi zao na kubadilishana uzoefu kati ya nchi ya Tanzania na nchi zingine kutokana na wahudhuriaji wa Mkutano huo hujumuisha watu kutoka mataifa mbalimbali na tunategemea ugeni wa nchi 50 Afrika".
Aidha ametoa rai kwa wasanii, wadau wa Muziki,wasambazaji na Meneja wa wasanii kuhudhuhuria Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika Novemba 9,2023 hadi Novemba 11 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam.
"Mkutano utawapa nafasi wadau wa muziki kuona namna gani wanauza kazi zao kwenye mitandao mikubwa ya kupakua muziki hivyo wasanii wajitokeze kwa wingi ili waweze kuuza kazi zao Kimataifa na wataalam wa maswala ya fursa na uwekezaji watakuwepo na kushiriki midahalo mbalimbali kwa siku 3."
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Music Afrika Eddie Hatitye amesema Mkutano huo utahudhuriwa na mataifa 50 lengo ni kubadilishana uzoefu katika kukuza Masoko ya Kimuziki.
Hata hivyo ameeleza namna Muziki wa singeli umeweza kuleta mabadiliko makubwa na kupelekea na Msanii Sholo Mwamba kunufaika kupitia Mkutano huo uliofanyika 2022 na hatimae kupata nafasi ya kushiriki Tamasha la muziki nchini Ujerumani mapema mwaka huu.
Aidha Hatitye amewaasa Wasanii wa muziki wa Singeli kujitokeza kwa wingi ili kuongeza wigo mpana wa kuuza na kusambaza muziki huo kwa wasambazaji na wadau wa Kimataifa kama muziki wa Bongofleva ulivyoweza kupenya mipaka ya Tanzania na kujizolea mashabiki wengi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...