Na. Mwandishi wetu Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha kuanzia Julai 01, 2023 hadi sasa kupitia operesheni mbalimbali dhidi ya madawa ya kulevya limefanikiwa kukamata Mirungi kilogramu 257.3, Bhangi kilogramu 98 pamoja na Heroine gramu 100.
Akitoa taarifa hiyo Agosti 18, 2023 Kamanda wa Polisi Mkoani humo Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo amesema mbali na madawa hayo pia wamefanikiwa kukamata watuhumiwa 32 wakiwa na pombe ya Moshi lita 238.5 pamoja na mitambo 04 ya kutengeneza pombe hiyo.
ACP Masejo amesema pia wamefanikiwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa 28 wa makosa ya ukatili na baadhi yao wamehukumiwa kwenda jela vifungo mbalimbali.
Kati ya waliohukumiwa, watuhumiwa 03 walihukumiwa kwenda jela vifungo vya maisha kwa makosa ya ubakaji na ulawiti na mtuhumiwa 01 alihukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kosa la ubakaji.
Kamanda Masejo amesema mafanikio hayo yametokana na elimu ambayo inaendelea kutolewa kwa wananchi ambao wamekua wakitoa ushirikiano kwa Jeshi hilo na kupelekea Mkoa huo kuendelea kuwa shwari hasa kwa kuzingatia ni kitovu cha Utalii Nchini.
Aidha ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu katika jamii ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Pia amewataka watu wachache wanaojihusisha na uhalifu kuacha mara moja vitendo hivyo kwani Jeshi hilo halitasita kuwakamata na kuchukua hatua za kisheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...