Njombe

Shirika la Posta mkoa wa Njombe limeingia mkataba wa utendaji kazi na wafanyakazi wake wa kufikia malengo ya msimu wa mwaka 2022 - 2023 ikiwemo kuzalisha milioni 406,huku pia watumishi wa mkoa huo wakipewa semina juu ya mambo mbalimbali ikiwemo afya na masoko.

Meneja wa Posta Njombe Lawi Mwaipopo amesema shirika hilo limekuwa na malengo makubwa ambayo ni lazima kutekelezwa ambapo kupitia malengo waliyopewa Posta mkoa wa Njombe ameona ipo haja ya kutoa semina kwa watumishi.

"Tuna malengo ambayo tumepewa na ni lazima tuyatimize cha kwanza ni uzalishaji ni lazima malengo tuyatimize tuna milioni 406 ya kuzalisha na kwa timu yetu hii tuliyo nayo mimi nina amini kabisa lazima tutaweza"amesema Mwaipopo.

Sambamba na hilo shirika hilo limetoa mafunzo mbalimbali ya ndani pamoja na ya nje ikiwemo mafunzo ya afya,masoko pamoja na bidhaa ya bima inayotakiwa kufanywa na shirika hilo mkoa wa Njombe ambapo tayari mikoa mingine imekwishaanza.

Nao baadhi ya watumishi wa shirika hilo wameshukuru uongozi kwa kuwakutanisha na kutoa semina ambapo pia wameahidi kwenda kuongeza juhudi ili kufikia malengo ambapo pia wametoa wito kwa uongozi kuboresha ofisi zao zikiwemo za Makambako na Ludewa ili kuboresha ufanisi katika kazi.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...