Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stegomena Tax (Mb) akifuatilia hotuba za ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambao ni maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo utakaofanyika Luanda, Angola tarehe 17 Agosti 2023.
Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa SADC aliyemaliza muda wake ambaye ni Waziri wa Ushirikiano wa Kikanda wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mhe. Antipas Nyamwisi akikabidhi uenyekiti wa baraza hilo kwa Waziri wa Uhusiano wa Nje wa Angola, Mhe. Téte António
Waheshimiwa Mawaziri wa SADC wakiendelea na mkutano wao ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo utakaofanyika Luanda, Angola tarehe 17 Agosti 2023


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...