Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
WASANII maarufu wa muziki wa Singeli Dulla Makabila pamoja na Shollo Mwamba wametambiana katika kuelekea mechi ya mashabiki wa timu za Simba na Yanga unaotarajiwa kuchezwa leo Agosti 25, 2023 katika Uwanja wa Paje Makunduchi visiwani Zanzibar.
Mechi hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa timu hizo kubwa nchini utahusisha mashabiki wa Simba na Yanga wanaoishi Makunduchi na lengo la mechi hiyo ni kunogesha tamasha la Kizimkazi ambalo linatarajiwa kuzinduliwa kesho na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi.
Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili Zanzibar Sholo Mwamba na Dulla Makabila kila mmoja amezungumzi mchezo kati ya mashabiki wa timu hizo huku kila mmoja akiahidi kuibuka na ushindi.
Katika mchezo huo Dulla Makabila amesema kama kawaida yuko upande wa timu yake ya Yanga na atakuwepo uwanjani akicheza namba anayocheza mchezaji wa Klabu ya Yanga Scudu Makudubele wakati Sholo Mwamba amesema atakuwa upande wa Simba na atacheza nafasi anayocheza Kibu Denis.
Kwa upande wake Dulla Mabilla amesema kuwa amejiandaa vya kutosha kuhusu mchezo huo unaofanyika leo ikiwa ni sehemu ya matukio kuelekea Tamasha la Nane la Kizimkazi."Sina shaka na uwezo wa mashabiki wa Yanga na leo tutashinda bao 5-0.
"Uzuri ukiwa Yanga kuanzia mchezaji anajua mpira lakini na shabiki naye anajua mpira, leo nikipata nafasi nitacheza.Kocha wa timu ya mashabiki wa Yanga Ally Kamwe kama ataamua kunipa nafasi nitacheza na niko tayari, nitacheza nafasi ya Scudo Makudele.
" Leo nataka kuonesha kipaji changu, ujue nimecheza sana mpira lakini baada ya kuumia nikaacha.Mashabiki wa soka waje uwanjani waone ninavyouchezea mpira, "amesena Dulla Makabila.
Aidha amesema wamejipanga vema kutoa burudani katika tamasha la Kizimkazi na ndio maana ameamua kuja huku akielezea kuwa anafahamu tamasha hilo ni la Mama Rais Samia Suluhu Hassan hivyo lazima afike kumsapoti.
Wakati Dulla Makabila akiyaeleza hayo, Shollo Mwamba amesema leo ataichezea Simba na kazi yake itakuwa kumzuia Dulla Makabila." Leo nataka kumuonesha Dulla Makabila kuwa niko vizuri kwenye soka.Kwa kuwa nina rasta nasi leo nitakuwa Kibu Denis."
Kuhusu tamasha la Kizimkazi Shollo Mwamba ametumia nafasi hiyo kuelezea umuhimu na ukubwa wa tamasha hilo na katika kuonesha kulisapoti yeye na Dulla Makabila wamekuja na watapanda jukwaa moja."Tulikuwa kwenye sherehe za Mwenge lakini tumeondoka na kuja huku kwenye jambo la Mama."
Kwa kukumbusha tu Tamasha la Kizimkazi limeandaliwa na kuratibiwa na Tasisi ya Mwanamke Initiatives ambayo Mwenyekiti wake ni Wanu Ameir Hafidh na kilele cha tamasha hilo kitakuwa Agosti 31 mwaka huu na mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...