Na.Khadija Seif, Michuzi Blog
WATANZANIA wametakiwa kuenzi utamaduni wa mtanzania aliyouacha Baba wa taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuwa na viongozi wenye kufanya kazi kwa weledi.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya mahafali ya 25 katika Shule ya awali na msingi ya Mwalimu julius Nyerere Mkuu wa shule hiyo Bi Maria Masai amesema wakati wa mwalimu uhai wake waasisi walimuomba watumie jina lake wakiwa na lengo la kufuata nyayo zake ,ikiwa pamoja na kutoa elimu bila kuwepo na ubaguzi wowote.
Wakati wa uhai wa hayati mwalimu Julius Nyerere alikutana na kuzungumza na waasisi wa shule hii ambao walimuomba watumie jina lake ambapo aliwaasa shule hiyo itoe elimu bora bila kubagua dini na ukabila .
Aidha,amesema shule hiyo inajivunia madili hayo mpaka sasa kwani wapo wanafunzi ambao ni watanzania na baadhi wakiwa ni wanafunzi kutoka mataifa mengine.
Pia ameeleza malengo yao mwaka huu ni kuhakikisha wanafunzi wao 45 ambao wafanya mtihani wa kumaliza kidato cha saba mwezi ujao wanafanya vizuri na kuendelea na elimu ya sekondari.
Amewapongeza wazazi pamoja na wahitimu hao kutokana na ushirikiano wanaowapa kipindi chote kuhakikisha wnatimiza ndoto zao kielimu.
Masai ametaja changamoto zilizopo shuleni hapo kuwa ni wazazi kushindwa kulipa ada kwa wakati jambo ambalo limekuwa likikwamisha maendeleo ya mwanafunzi, na kuiomba serikali ipunguze kodi kwa shule binafsi ili iwarahisishie shuhuli za uendeshaji wa shule.
Nae Mkurugenzi wa shule hiyo Salva Rweyemamu ameiomba serikali ipunguze kodi kwa shule binafsi ili kuwarahisishia waweze kufanya shuhuli za uendeshaji.
"Tunaiomba Serikali itupunguzie kodi katika shule za sekta binafsi ili na sisi tuweze kutoa elimu bora.
Amewataka wahitimu hao kuongeza juhudi katika masomo ili wapate nafasi ya kujiunga na elimu ya sekondari.
"Ninawapongeza walimu kwa kazi kubwa wanayoifanya kuhakikisha kila mwanafunzi anapata matokeo mazuri ninaomba wazazi tuongeze ushirikiano.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...