Na Said MMwandishi Wetu, Zanzibar

HAKUNA Mbabe !Ndivyo unavyoweza kuielezea mechi ya mashabiki wa Simba na Yanga wanaoishi Makunduchi visiwani Zanzibar baada ya mchezo wao kumalizika kwa sare ya mabao 10-10.

Mchezo huo uliokuwa na msisimko mkubwa kutokana na ushindani wa timu zote mbili umefanyika Paje Makunduchi na maelfu ya wananchi wamejitokeza kuushuhudia mechi kati ya mashabiki wa Simba na Yanga ambao ulitawaliwa na tambo nyingi za makocha ambao ni Ally Kamwe kwa upande wa Yanga na Ahmed Ally kwa upande wa Simba.

Katika mchezo huo ulioanza saa 10 jioni wachezaji wa timu zote mbili walionesha ubora wa vikosi vyao lakini kubwa zaidi vipaji vya soka walivyonavyo wachezaji wa Makunduchi.

Wakati wa mchezo huo unaendelea ulikuwa na kasi, akili na mbinu za kila lakini timu ya mashabiki wa Yanga ilifanikiwa kupata bao la mapema ambalo lilidumu kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Yanga kutangulia katika mchezo huo uliokuwa wa vuta ni kuvute ulimfanya Kocha wao Ally Kamwe kutokuwa na presha lakini kwa Ahmed Ally presha ilionekana kuwa juu na kadri muda ulivyozidi kwenda Simba walianza kuuteka mchezo hali iliyosababisha Kamwe kusimama mara kwa mara kutoa maelekezo kwa wachezaji wake.

Hata hivyo Simba walionekana kufanya mabadiliko ya wachezaji mara kwa mara huku Yanga wakifanya mabadiliko ya wachezaji wake bila haraka.

Pamoja na hayo , hadi timu zinakwenda mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa bao moja.Baada ya mapumziko timu zikarejea uwanjani kuendelea na dakika zilizobakia na mchezo ulianza kwa kasi lakini Simba walionekana wakipamba kuhakikisha wanasawazisha.

Hivyo kabla ya dakika 15 mchezo huo kumalizika Simba walifanikiwa kupata bao na kuufanya mchezo huo kuwa na sare ya bao 1-1 hadi dakika 90 zinamalizika.

Kutokana na matokeo hayo timu hizo zikaingia kwenye mikwaju ya penalt ambapo Yanga walianza kwa kukosa penalt yao ya kwanza na Simba wakapata penalt yao.

Yanga wakaenda kupiga penalt yao ya pili wakapata na Simba walipopiga penalt yao ya pili wakakosa.Hivyo ikawa kila timu imekosa moja na imepata moja na kuanzia hapo kila timu ikawa ikipiga inapata na walipofika penalt tisa mwamuzi alipiga fimbili ya kumaliza mchezo.

Hivyo ikaamriwa mchezo huo utarudiwa tena Agosti 31 mwaka huu ambapo mgeni rasmi Dk.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kushuhudia mechi ya Simba na Yanga ya Makunduchi ambapo pia ndio itakuwa siku ya kilele cha Tamasha la Nane la Kizimkazi.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo Waziri Mchengerwa amesema katika mchezo wa marudiano Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia anatarajiwa kuwa uwanjani kushuhudia mchezo huo pamoja na kutoa zawadi kwa mshindi ambapo mshindi atachukua kombe na Sh.milioni tano na mshindi wa pili ataondoka na kitita cha Sh.milioni tatu.

Katika mchezo wa jana wa timu hizo mbali ya wananchi pia  ulishuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mchengerwa, Viongozi wa Mkoa wa Kusini Unguja pamoja na Mwenyekiti wa Mwanamke Initiatives Foundation Wanu Ameir Hafidh ambao ndio wadhamini  wakuu mchezo huo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...