Na Humphrey Shao,Michuzi TV
SHRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limefanya mageuzi makubwa ambayo yameliwezesha shirika hilo kuongeza mapato kutoka Sh.bilioni 1.3 hadi Sh bilioni 61.1 ambalo ni sawa na ongezeko la asilimia 4425.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dkt.Venance Mwasse wakati wa kikao kazi kati ya shirika hilo na wahariri wa vyombo vya habari nchini chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Amesema, mafanikio hayo yameliwezesha shirika sasa kuanza kutoa gawio serikalini, kwani tangu lianzishwe mwaka 1972 lilikuwa halijawahi kupeleka kitu chochote serikalini.
Amefafanua sababu zilizowawezesha kufikia mafanikio hayo ni kwa kubadili fikra,ushirikishwaji, nidhamu, kujiwekea malengo na kuyatekeleza.
“Kwa ujumla, tulifikia mahali ikabidi tubadilike kifikira, kuna mashirika ya umma yanayotoa huduma na kuna mashirika ya umma yanayotakiwa yajiendesha kibiashara.
“Kwa hiyo tulipoamua kujiendesha kibiashara, tukaamua sasa kwenda kuzitafuta fursa, tulipobonyeza hiyo button tukaona mambo yamekwenda. Viongozi kwa kulitambua hili ni shirika la umma nikaona lazima tuumize vichwa.
"Pamoja na kuongeza morali ya wafanyakazi kwa kuona wanajaliwa na mipango iwe inanyooka, " amesema na kuongeza STAMICO litaendelea kusimamia shughuli zake kikamilifu ili kuongeza tija katika shughuli zinazotokana na madini.
Aidha amesema kuna miradi mingine inayosimamiwa na Shirika hilo ambayo ni pamoja na mradi wa mkaa mbadala wa kupikia kwa kutumia makaa ya mawe, mradi wa dhahabu STAMIGOLD unaomilikiwa na serikali kwa hisa asilimia 99 na Msajili wa Hazina hisa asilimia 1.
Pamoja na kiwanda cha kusafisha Dhahabu Mwanza ambacho kinamilikiwa na Shirika hilo kwa asilimia 25 na Mbia asilimia 75.“Uanzishwaji wa kiwanda hicho umesaidia, kusafisha dhahabu na mazao ambatano, uhaulishaji wa Teknolojia, kuongeza huduma kwa Jamii (CSR), mapato kwa serikali.
Dkt. Mwasse amesema STAMICO limetoka kuwa Shirika linalotengeneza hasara hadi kutengeneza faida na wamelipa gawio kwa serikali jumla ya Sh.bilioni 8, hivyo wameondoa utegemezi wa ruzuku kutoka serikalini.
Amesema wamepata hati safi kwa miaka 3 mfululizo kutokana na ukaguzi wa mahesabu, lakini mapato ya ndani yameongezeka kutoka Sh.bilioni 1.3 kwa mwaka 2018/19 hadi Sh.bilioni 61.1 kwa mwaka 2022/23.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...