Njombe
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,Tulia Ackson ametoa wito kwa watanzania kutafuta majibu ya hoja walizonazo kwa kufuata utaratibu na njia sahihi lakini sio kwa njia za kwenda barabarani.
Dkt,Tulia ameeleza hayo wilayani Makete mkoani Njombe wakati akizungumza na wanaCCM kwenye mkutano mkuu wa jimbo wa wilaya hiyo uliokuwa maalum kwa ajili ya uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kipindi cha mwaka 2020 - 2023 chini ya mbunge wa jimbo hilo Festo Sanga.
"Mwananchi mwenzangu usikubali mtu anayetaka kuchochea vurugu tutaathrika sote kama liko jambo halieleweki kwenye jamii,serikali imeweka viongozi hadi kwenye ngazi ya kitongoji nenda ukaulize huko kama hupati majibu muwakilishi wako yuko hapa kama kwa mbunge ni mbali nenda kwa diwani,hujamuona nenda hata kwa mtendaji tafuta majibu ya hoja zako sio barabarani"amesema Tulia
Tulia ameongeza kuwa "Mahakama ya kikatiba iliyokuwa imeundwa kwa ajili ya kesi waliyopelekea mahakamani imeshatoa hukumu,imesema hawana hoja sasa Mahakama ndio chombo cha kutoa haki kimesema hawana hoja wao kama wanataka wakate rufaa ndio utaratibu,wameshatoka tena kwenye mstari wako huko nje wanahamasisha watu sasa jamani hoja yenu nyie ni bandari au mna jambo lingine"aliongeza Tulia
Kauli ya Spika imekuja muda mchache baada Kamanda wa Polisi Tanzania,IGP Camilius Wambura kuwataka wanaondaa maandaamano nchi nzima ili kuiangusha serikali kusitisha mara moja kwa kuwa jambo hilo ni uhaini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...