Na Mwandishi wetu.
Tamasha la nane la Utalii na wanahabari la Arusha (Arusha tourism Festival ) linatarajiwa kufanyika kwa siku tatu Octoba12 hadi 14, 2023 jijini Arusha kwa kuwashirikisha wanahabari mikoa 10 nchini na wadau wa sekta ya Utalii na Uhifadhi nchini.
Tamasha hilo, linaandaliwa na Taasisi ya Arusha Media kwa kushirikiana na Taasisi ya wanahabari ya MAIPAC na Chama cha waandishi wa habari za michezo (TASWA).
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mratibu wa Tamasha hilo, Mussa Juma, amesema tamasha la mwaka huu, litakuwa na matukio matatu, Maonesho ya bidhaa za Utalii, Kongamano kuhusu sekta ya Utalii na Uhifadhi na michezo (Media Day Bonanza)
“Tunatarajia kushirikisha watu zaidi 700, wakiwepo wafanyabiashara wa sekta ya Utalii, Wataalam wa utalii na Uhifadhi na waandishi wa habari kutoka mikoa 10 nchini ambayo imekuwa na changamoto ya migogoro baina ya wanyamapori na binaadamu” amesema.
Juma amesema Octobar 12-14 kutakuwa na Maonesho, Octoba 13 kongamano la wadau wa Utalii na Octobar 14 kutakuwa na michezo ambayo itashirikisha timu za Wanahabari na wadau wa Utalii.
“Tumeanza maandalizi ya Tamasha hili na mwaka huu, limeboreshwa zaidi tofauti na miaka ya nyuma na tunatarajhia kuwakutanisha wadau wa sekta ya Utalii na Uhifadhi na wanahabari ili kuwajengewa uwezo masuala mbali mbali ya Utalii na uhifadhi,” amesema.
Juma amesema Katika Tamasha hilo, ambalo tangu mwaka 2015, limekuwa likifanyika kauli mbiu mwaka huu, kupunguza migogoro baina ya wanyamapori na wananchi lakini pia kutakuwa na mada ya kadhaa ikiwepo Ulinzi wa maeneo ya mapito ya wanyamapori, kuzuia biashara haramu ya wanyamapori na nyamapori na umuhimu wa vyombo vya habari kukuza sekta ya Utalii .
“Tamasha hili linatarajiwa kusaidia kukuza sekta ya Utalii na Uhifadhi lakini kujenga uelewa mzuri kwa wanahabari juu ya mafanikio na changamoto za sekta hii lakini pia kwa kuwa tutakuwa katika maadhimisho ya kumbukumbu tangu kifo cha baba wa Taifa Mwalimu Nyerere tamko lake juu ya uhifadhi na Wanyamapori la mwaka 1961 linatajadiliwa,” amesema.
Juma amesema wataalikwa watendaji wa Taasisi za Uhifadhi na Utalii, Shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori (TAWA) Taasisi ya Utafiti wa wanyamapori (TAWIRI), Jumuiya za hifadhi za Wanyamapori (WMA) Wakala wa Misitu na Nyuki (TFS) na Wawekezaji katika sekta ya Utalii.
“Tutaendelea kutoa taarifa juu ya maandalizi ya tamasha hili la Utalii na tunaomba wadau mbali mbali kuendelea kujitokeza kuliwezesha na kushiriki,” amesema.
Ngoma za utamaduni katika tamasha la Arusha Tourism Festival zikiwaburudisha wageni mbalimbali.
Awali Mratibu wa Arusha Media, Andrea Ngobole akizungumzia michezo itakayofanyika Octobar 14, alisema kutakuwa na mchezo wa soka, mpira wa pete,kuvuta kamba, kukimbiza kuku na mbio za magunia.
“Kama mnakumbuka timu ya TASWA FC Dar es Salaam ndio walikuwa mabingwa watetezi katika tamasha la saba katika soka na mpira wa pete tayari wamethibitisha kuja kutetea ubingwa wao,“ amesema.
Ngobole amesema zawadi za mwaka huu,zitatangazwa hivi karibuni sambamba na wadhamini wote ambao watakuwa wamejitokeza.
Timu ya michezo ya waandishi wa habari za michezo wa Dar es Salaam TASWA FC ambao ni mabingwa watetezi wa Tamasha lililopita wamethibitisha kushiriki tena katika tamasha hili mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...