Prophet Suguye akiwa anaongoza 13/82023 Ibada katika Kanisa la WRM Kivule amewakumbusha Waumini wake juu ya UNABII aliotoa March 26,2021 alipotabiri juu ya masuala ya Kiuchumi na kuwataka wajiandae kwa fursa mbalimbali na kuwa matajiri.
“Mwaka 26 March 2021 tukiwa katika wiki moja au mbili wakati Magufuli amelala nilitoa utabiri nikawaambi jifunzeni Kiingereza, Kifaransa, jifunzeni lugha mbalimbali mpaka za Kichina”
“Nikasema kuna mataifa yanakuja yatakaa katika Nchi yetu yatakuwa tayari kufuata Sheria zetu, watafanya kazi na tutakuwa Matajiri sana huu ni wakati wa Baraka ndio wakati msipokuwa makini mnaweza kupigana hovyo”
“MUNGU anapoachilia baraka ndipo na maadui wanainuka kupambana na Baraka zenu, Hakuna wakati wa hatari kwako kama muda wa kufanikiwa saivi kila Mtu anaitama i Tanzania na kila propaganda zinainuka Tanzania”
“Amka Tanzania huu ni wakati wetu sio wakati wa kurumbana na kuvunjana moyo, Tanzania ipokee Wachina, Waarabu, Wafaransa, Wakorea, ipokee Waafrika wenzao kama wana uwezo wa kuwekeza na wakafanya vitu vizuri na wakafuata Sheria zetu hatuna haja kuwachukia waje
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...