Na Mwandishi wetu.
KIKOSI cha timu ya Taifa cha mchezo wa Pooltable leo kimeanza rasmi kambi baada ya tangazo la kutajwa sambamba na kuitwa kambini wachezaji 17 watakaoingia katika mchujo wa kupata kikosi kitakachowakilisha Nchi kwenye mashindano ya Afrika(AAPA) yanayotarajiwa kufanyika Octoba mwaka huu Nchini Afrika Kusini.
Akizungumza na wachezaji wakati wa kikao kifupi cha kukalibisha Wachezaji Kambini, Meneja wa timu ya Taifa, Patrick Nyangusi alisema anategemea kuona mambo mapya na mazuri katika kambii hii kwa mjuano wa kupata nani sahihi wa kuwakilisha nchi, naomba kila mtu ajitume kwa kadri ya uwezo wake ili mpaka tupate changamoto za kuchagua nani aende Afrika Kusini na nani abaki.
Nae Kocha wa timu ya Taifa, Denis Lungu aliwakaribisha kambini Wachezaji na kuwaambia wazi kuwa uwezo wako ndio utakupeleka Afrika kusini au kubaki Tanzania na kutuangalia mitandaoni,
Alisisitiza Lungu, sitambeba mchezaji bali mchezaji ajibebe kwa uwezo wake kuanzia leo katika kambi hii.Muda tulionao ni mchache sana lakini kwasababu kambi hii si ya kufundisha mchezaji kucheza naamini haitakuwa ngumu.
Lungu alimaliza kwa kuwakaribisha wachezaji wote kambini waliopata bahati ya kuteuliwa na kuwatahadhalisha kuwa wasijione kuwa bora kuliko walioachwa bali wao wameonekana wanaweza kuwakilisha Nchi wa vigezo vilivyoangaliwa na Viongozi wa chama cha Pool Taifa(TAPA).
Afisa habari wa Chama cha Pool Taifa, Lilian aliwataja wachezaji walioripoti kuwa ni Seif Hamadi, Festo Yohana, Issaya Paul, Abdallah Hussein, Mussa Mkwega, Innocent Sammy, Melkizedeck Amadeus, Norbeth Kobelo, Jackson Steven, Charles Venance, Anthon Thomas, Said Jumanne, Abdallah Miraji, Aboubakar Salum na Abdul Said Kiande
Wachezaji ambao mpaka sasa hawajaripoti ni Baraka Jackson kutoka Manyara na Yasin Athuman kutoka Dodoma ambao wataripoti kesho Kambini.
Lilian alisema kuwa kambi itakuwa katika klabu ya Snipers Mwenge Mpakani jijini Dar es Salaam na kama kutakuwa na mabadiliko yoyote watatoa taarifa.Muda wa mazoezi yatakuwa yanaanza saa kumi jioni na kuendelea.
.jpg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...