Na Said Mwishehe, Michuzi TV- Zanzibar

KUMEKUCHA Kizimkazi! Hivyo ndivyo unavyoweza kuzungumzia kuelekea Tamasha la Nane la Kizimkazi ambapo kabla ya kuanza kwa tamasha hilo Agosti 26, 2023 , mashabiki wa timu za soka za Simba na Yanga zilizoko mkoa wa Kusini Unguja Visiwani Zanzibar, zinatarajia kumenyana vikali.

Timu hizo zinatarajia kuingia dimbani Ijumaa ya Agosti 25, 2023 ambapo mgeni rasmi katika bonanza la  mchezo huo anatarajiwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mohamed Mchengerwa.

Tayari makocha wa timu hizo ambao ni Ahmed Ally kwa upande wa Simba na Ally Kamwe kwa upande wa timu ya Yanga wametoa tambo zao na  kila mmoja akiahidi timu yake kuibuka na ushindi.

Akizungumza leo Agosti 22, 2023 katika eneo la Makunduchi,  Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke Initiative ambao ndio waratibu wa Tamasha la Nane la Kizimkazi Wanu Hafidh Ameir ameeleza katika kuelekea tamasha hilo kutakuwa na matukio mbalimbali na moja ya tukio ni bonanza ambalo litazikutanisha timu za mashabiki wa Simba na Yanga.

Amefafanua mechi ya mashabiki wa klabu hizo mbili kubwa hapa nchini imekuja mahususi ikiwa ni ushereheshaji katika kuelekea Kilele cha tamasha la Kizimkazi, ambalo pia limelenga kuongeza hamasa ya mashabiki kwa timu zao

"Katika kuelekea Tamasha la Nane la Kizimkazi tutakuwa na bonanza la mpira wa miguu ambapo mashabiki wa timu za Simba na Yanga watachuana ikiwa ni sehemu ya bonanza kuelekea kwenye uzinduzi wa tamasha letu ambalo litafanyika Agosti 26, 2023...

" Na mgeni rasmi katika ufunguzi wa tamasha la Kizimkazi  anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi na kilele cha tamasha hili kitakuwa Agosti 31 mwaka huu na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan, "amesema Wanu.

Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja visiwani Zanzibar  Rashid Hadid Rashid amesema Tamasha la Nane la Kizimkazi limezidi kushika kasi nchini na limekuwa kichocheo  katika kuimarisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo na kijamii kama ilivyo azma ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.

Amefafanua tamasha hilo licha ya kutoa burudani kama ilivyozoeleka, wanatarajia litajikita pia katika kutoa misaada ya kijamii na kiutu kwa wananchi wa makundi yote yakiwemo yenye uhitaji maalum.

Kwa upande wa makocha wa timu hizo Ahmed Ally na Ally Kamwe pamoja na kutoa tambo zao , wametumia nafasi hiyo kuzungumzia umuhimu na upekee wa tamasha hilo na kwamba wanaliunga mkono na watahakikisha linakuwa la kitaifa na kimataifa.Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Visiwani Zanzibar Rashid Hadid Rashid(katikati) akizungumza kuhusu Tamasha la Nane la Kizimkazi linalotarajia kuanza Agosti 26, 2023
Kocha wa timu ya mashabiki wa Yanga Kizimkazi Ally Kamwe akizungumza kuhusu maandalizi ya timu yake kuelekea mchezo kati yao na timu ya mashabiki wa Simba.
Kocha wa timu ya mashabiki wa Simba Kizimkazi,Ahmed Ally akizungumza kuelekea bonanza la mchezo kati ya timu yake na mashabiki wa timu ya Yanga unaotarajia kufanyika Agosti 25, 2023 ikiwa ni kuweka hamasa kuelekea tamasha la Nane la Kizimkazi linalotarajia kuanza Agosti 26, 2023 visiwani Zanzibar.
Kocha wa timu wa mashabiki wa Simba Ahmed Ally akiwa na mashabiki wa timu hiyo leo baada ya kuzungumzia mchezo kati yao na timu ya mashabiki wa Yanga

Kocha wa timu wa mashabiki wa Yanga Kizimkazi Ally Kamwe  akiwa na mashabiki wa timu hiyo leo baada ya kuzungumzia mchezo kati yao na timu ya mashabiki wa Yanga

Makocha wa timu za mashabiki wa Simba na Yanga walioko Makunduchi ambao pia ni wasemaji wa Klabu hizo Ahmed Ally ( wa pili kushoto) na Ally Kamwe wa Yanga(wa nne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa taasisi ya Mwanamke Initiatives Wanu Hafidh  Ameir (wa kwanza kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadid Rashid( wa tatu kushoto)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...