Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amemshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake ya dhati ya kuendeleza sekta za uzalishaji za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili ziweze kuwa na manufaa makubwa kwa Wananchi na Taifa kwa ujumla.
Waziri Ulega ametoa shukrani hizo leo Agosti 11, 2023 ofisini kwake jijini Dodoma wakati akifanya mahojiano maalum na waandishi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC).
Alisema kwa mara ya kwanza katika kipindi hiki cha Maonesho ya NaneNane imeshuhudiwa kuwa sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi zimejadiliwa kwa mapana sana na watu wa rika na jinsia zote, hiyo yote imetokana na msukumo wake Mhe. Rais wa kutaka sekta hizo za uzalishaji zikuwe na kuleta tija na manufaa kwa wananchi.
"Tunamshukuru sana Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupa nguvu, baraka na maelekezo, tunahisi fahari kubwa sana kufanya kazi chini ya maelekezo yake, alisema huku akiongeza kuwa, sio jambo rahisi kumpata Mhe. Rais kufanya kazi ya kutembelea mabanda kwa masaa zaidi ya nane," alisema
Aliongeza kuwa kitendo cha Mhe. Rais kutumia siku nzima kwenye maonesho ya NaneNane inaonesha wazi juu ya utayari wake wa kuzisogeza mbele hizi sekta za uzalishaji ili ziweze kuwa na manufaa makubwa katika Taifa letu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...