Viongozi wanaotokana na Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini wametakiwa kuepuka kutawaliwa na tamaa wanapokuwa madarakani ili kulinda sifa ya uongozi na Chama hicho.
Wito huo umetolewa na katibu wa idara ya siasa na organaizesheni wa jumuiya ya wazazi wa Chama cha Mapinduzi taifa Said King'eng'ena wilayani Njombe wakati wa mafunzo maalum kwa viongozi wa jumuiya hiyo na jumuiya nyingine.
"Viongozi wa leo wanatuharibia Chama chetu kwasababu ya tamaa wanazitumia nafasi za uongozi kama nafasi za kupigia besenga kwa watu kwa hiyo tunatamani kuwa na aina ya viongozi wanaotosheka na wasiokuwa na tamaa kwasababu ndio inayotia aibu Chama chetu"amesema King'eng'ena
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo wilaya ya Njombe Clemence Malekela amesema anaamini mabadiriko makubwa yanakwenda kupatikana kupitia mafunzo waliyopata.
"Mafunzo haya yakawe sasa ni chachu ya kukutoa pale ambapo tulikwama hivyo ninaamini kupitia haya mafunzo sasa watafanya mabadiriko ndani ya jumuiya yetu"amesema Malekela
Ikiwa kazi kubwa ya kiongozi ni kuongoza watu wenye afya njema ili kukuza uchumi wa watu na pato la taifa,kabla ya mafunzo hayo kumekuwa na zoezi la upimaji wa afya kwa wananchi bure pamoja na uchangiaji wa damu ambapo miongoni mwa wananchi akiwemo Joshua Mahenge,Paulina Mkane na Amos Mwasamala wamejitokeza kupima afya zao na kutoa rai kwa wengine kuendelea kupima afya ili kukabiliana na magonjwa pindi wanapoyabaini.
Katibu wa idara ya siasa na organaizesheni wa jumuiya ya wazazi wa Chama cha Mapinduzi taifa Said King'eng'ena akiendelea na semina kwa Jumuiya ya wazazi na jumuiya zingine waliojitokeza katika ukumbi wa turbo mjini Njombe.
Mwenyekiti wa Jumuya ya wazazi wilaya ya Njombe Clemence Malekela akitoa shukrani kwa muwezeshaji wa semina mara baada kupewa mafunzo mbali mbali ya uongozi na kuahidi kwenda kufanya mabadiriko makubwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...