Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kipunguni pamoja na Mtandao wa Kutokomeza Ukeketaji Tanzania wamekuja na mpango mkakati utakaowashirikisha wadau mbalimbali kwenye jamii ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea ya kumaliza kabisa suala hilo kwa kushiriakiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) toka mwaka 2013.
Akizungumza wakati wa mafunzo Mwenyekiti wa Mtandao wa Kutokomeza Ukeketaji Tanzania Joseph Selasini amesema wamekuja ili kujifunza masuala mbalimbali ya kiuchumi yanayoendeshwa na Kituo hicho ambapo watumia raslimali hizo ili kupambana na ukatili wa kijinsia ambapo kuna ugumu mkubwa sana kwenye suala la kuzuia ukeketaji kwani watu wanataka kulinda mila na desturi za kwao hivyo basi tunataka kutokomeza na sio kupambana na ukeketaji.
Amesema kama kweli tunataka kutokomeza ukeketaji inabidi kuelimishi hasa kwenda kwenye chimbuko kwa kuwauliza wakeketaji kuhusu uelewa wao kwenye suala la ukeketaji hasa kwenye faida pamoja na hasara ili wao waweze kuzungumza kiundani suala hilo ambapo tutaweza kutoa elimu kulingana na wao walichokisema na sio kwenda kufundisha mambo yaliyoandikwa kwenye vitabu.
Katika kutoa elimu inabidi kutumia wale watu walioko kwenye jamii hasa wakina mama waliopitia ukeketaji ili kuweza kutoa elimu ya kutosha kwani wao ndio wanajua hasara za ukeketaji na njia hi itasaidia kuweza kuamsha utambuzi kwenye jamii mfano ukitaka kwenda kutoa elimu kwa wamasai wanadharau maana wanakutazama kama wewe ni mrefu kuliko ukiwa mfupi kuliko wao au ukiwa mwanamke hawakusikilizi hivyo basi inabidi tuendane na mazingira husika.
Amesema lazima tujue ni mbinu gani tunaweza kuzifanya ili watu waweze kusema Mangariba ni watu wa aina gani na wakituambia kuwa wale ni mangariba usiende kutaja kuwa huyu ni ngariba kwani ukifanya hivyo hutoweza kuwapata watu kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu masuala ya ukeketaji mfano tunapokwenda shuleni tunawapa wanafunzi kila mmoja karatasi ili kuandika majina ya watu wanaokeketa kwa usili ili kupata taarifa iliyo nzuri na kuwaepusha kupata changamoto yoyote.
Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kipunguni Fatma Abduirahman Talib amesema hakuna kusema tunaweza kutumia polisi au Serikali kutumia sheria ili kuweza kumaliza ukeketaji kwasababu suala hili linahusiana na elimu pamoja na imani ya eneo husika hivyo inatakiwa kutumia zaidi busara ili kuweza kumaliza kabisa suala la ukeketaji hapa nchini.
"Nina furaha kuona taasisi mbalimbali kuja kujifunza masuala ya uchumi yanayoendana sambamba na kupambana na ukatili wa kijinsia kwani kuja kwenu ni kuendelea kutupa hamasa ya kufanya mambo makubwa hasa kwenye kupambana na suala la ukeketaji ili kuweza kulitokomeza kabisa. Alisema Fatma
Pia amesema kituo hicho kinapofanikiwa kuwaokoa watoto wa kike kwenye suala la ukeketaji wameanzisha mradi ili wasichana hao wajifunze masuala ya kilimo ili kuweza kujikimu kimaisha pamoja na wasichana wengine kuwasimamia kuendelea masomo pale wanapokimbia ukeketaji nyumbani kwao.
Pia amesema kunaaadhi ya Sheria za hapa nchini kufanyiwa marekebisho kwa kuwashirikisha wanasiasa kwenye suala hili la ukeketaji hasa kwenye maeneo ambayo yanaongoza kwa ukeketaji katika jimbo la Ukonga ili kujua ukubwa wa tatizo ilo ili kuja na mkakati wake wa kuwenda kulizungumzia Bungeni ili kuja na mabadiliko ya sheria hizo.
Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Kipunguni, Rozina Soka amesema kwa pamoja tunapotoka hapa haya maazimio yakasimamiwe kila mtu kwa nafasi yake ambapo polisi asimame kwenye nafasi yake, viongozi wa dini wakasimame kwenye nafasi zao, mwanahabari asimame kwenye nafasi yake, wanaharakati pia nao wasimame kwenye nafasi yake pamoja na viongozi wa serikali ili kuweza kutokomeza ukeketaji hapa nchini.
“Kabla ya kutoa taarifa sehemu inabidi kuangalia ni nani unampelekea taarifa hiyo kama ni sahihi na je hilo jambo litatuliwa kwa wakati na mtu huyo ukishakuwa na mashaka naye tafuta sehemu nyingine ya kupeleka taarifa hiyo kwa kushirkiana hasa kwa kupeana taarifa na kuomba ushauri utakaosaidia kutatua changamoto ya ukeketaji hapa nchini alisema Rozina.
Mlezi wa Kituo cha taarifa na Maarifa cha Kipunguni,Selemani Bishagazi(wa kwanza kulia) akitoa maelezo kuhusu namna Kituo hicho kilivyojidhatiti kwa kuwa na miradi mbalimbali ikiwemo hii ya kilimo cha mbogamboga kinachomilikiwa na wasichana waliokimbia masuala ukatili wa kijinsia hasa suala la Ukeketaji ili kujipatia kipato na pia.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Kutokomeza Ukeketaji Tanzania Joseph Selasini akizungumzia mikakati waliyojiwekea ili kuweza kupambana na ukeketaji hapa nchini pamoja na kueleza namna walivyojifunza mambo mengi yanayofanywa na Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kipunguni walipotembelea kituo hicho ili kujiongezea ujuzi.
Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kipunguni Fatma Abduirahman Talib akizungumza kuhusu namna wanavyoshirikiana na wanajamii wakiongozwa na Mwenyekiti wa mtaa pamoja na Polisi kata ili kuweza kutokomeza masuala yote ya ukatili hasa suala la Ukeketaji
Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Kipunguni, Rozina Soka akizungumza kuhusu namna jamii inavyobidi kushirikiana ili kuweza kutokomeza Ukeketaji hapa nchini wakati wa kikao cha kujadili na kuonesha kazi mbalimbali zinazofanywa na Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kipunguni.
Mlezi wa Kituo cha taarifa na Maarifa cha Kipunguni,Selemani Bishagazi akitoa maelezo kuhusu kazi za kiuchumi wanazozifanya kwenye Kituo hicho kwa wageni mbalimbali kutoka Taasisi na Mashirika mbalimbali ikiwemo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) waliofika ili kujifunza kazi mbalimbali za kiuchumi zinazoenda sambamba na ukatili wa kijinsia hasa Ukeketaji kwa watoto wa kike.
Mhasibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kipunguni , Livia Mhagama akisoma ripoti ya kutokomeza ukeketaji kwenye kituo hicho kuanzia mwezi Novemba mwaka 2022 hadi Juni, 2023 ambapo wameweza kutoa elimu kwa wanajamii 490 kuhusu madhara ya ukeketaji na kuweza kufanikisha kuokoa wasichana 14 ambapo wasichana wapya watatu walipokelewa kwenye nyumba salama.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Green Kids and Youth Vaileth Mwazembe akizungumzia namna taasisi hiyo inavyoweza kutoa elimu mashuleni pamoja na mitaani ili kuwajengea uelewa kuhusu ukatili wa kijinsia hasa kwenye masuala ya kujitambua na kuelewa madhara yatokanayo na ukeketaji wakati wa kikao kazi cha kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kipunguni walipotembelea kituo hicho ili kujiongezea ujuzi.
Sajenti Peter Mwankusi(kulia) akieleza namna wanavyoshirikiana na wanajamii katika hasa viongozi wa vituo vya Taarifa na maarifa katika kupinga ukatili wa kijinsia na namna wanavyowachukulia hatua za kisheria pamoja na kutoa elimu kwa jamii ili kuweza kutambua madhara yatokanayo na ukatili wa kijinsia hasa Ukeketaji.
Mkurugenzi wa Shirika la Himiza Prisca Ngweshemi akieleza namna anavyoshirikiana na Vituo vya Taarifa na Maarifa kikiwemo cha Kipunguni ili kuweza kutokomeza ukeketaji hapa nchini.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Magole kata ya Mzinga, Abdul Machungi akieleza namna anavyoshirikiana na Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kipunguni kwenye suala la kupambana na ukeketaji kwenye mtaa wake kwani mtaa huo umekuwa na matukio mengi ya Ukeketaji japo ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika kutekeleza majukumu yake.
Baadhi ya wadau mbalimbali wakichangia mada
Mkutano ukiendelea
Elimu ikiendelea kutolewa kwenye baadhi ya mashamba ya mboga zinazomilikiwa na wasichana waliokimbia ukatili wa kijinsia
Wageni wanitembelea mashamba ya mbogamboga ya Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kipunguni
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...