Na Janeth Raphael- MichuziTv - Dodoma.

TAASISI ya kudhibiti ubora wa mbegu Tanzania (TOSCI) imewataka wakulima na jamii kwa ujumla kutumia mbegu zilizothibitishwa ubora ili kuongeza mavuno, tija na kipato.

Hayo yamebainishwa na Mkurungezi Mkuu wa TOSCI, Patrick Ngwediagi, Agosti 15,2023 jiji Dodoma , wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo na mwelekeo wa mwaka wa fedha 2023/24.

Amesema ili kilimo kuwa na tija nchini wakulima wanapaswa kutumia mbegu zenye ubora na zilizothibitishwa na taasisi hiyo ili kuongeza mavuno na kipato.

"Wito wangu kwa wakulima na jamii kwa ujumla tumieni mbegu zilizothibitishwa ubora ili kuongeza mavuno,tija na kipato badala ya kuendelea kutumia mbegu ambazo hazina ubora na kupunguza tija kwenye kilimo nchini"amesema

Akizungumzia mafaniko Mkurugenzi huyo ametaja udhibiti wa mbegu feki kuwa ni fanikio mojawapo ililolipata katika uongozi wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ambapo imeshinda kesi tano ilizozipeleka mahakamani.

Aidha kutokana na sera nzuri na usimamizi mzuri TOSCI imefanikiwa kuwashawishi wazalishaji wa mbegu kuzalisha mbegu hapa nchini kwa asilimia 81 tofauti na ilivyokuwa awali ambapo mbegu zilizalishwa kwa asilimia 35.

Pamoja na hayo amesema utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2023/24 watatumia kiasi cha Sh.bilioni 12.6 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali.

Amesema moja shughuli watakayo ifanya ni kuendelea na uboreshaji wa shughuli za utafiti na usimamizi wa ubora wa mbegu"Taasisi itaendelea kuboresha shughuli za uthibiti na usimamizi wa ubora wa mbegu zilizoanzishwa katika mwaka wa fedha uliopita katika maeneo mbalimbali"amesema.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...