Na Mwandishi wetu- Ngorongoro


Wazee wa kimila jamii ya Maasai na viongozi wa dini katika wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha, wamelaani kitendo cha waandishi wa habari na watumishi wengine wa serikali kushambuliwa.Tukio hilo lilitokea Agosti 15 mwaka huu katika kijiji cha Enduleni wakati watumishi wa serikali na waandishi wa habari wakiwa katika majukumu yao.


Viongozi hao kwa pamoja wakiwa wamekutana katika kijiji cha Kapenjiro, wamesema wamemuomba Mungu aweze kuwasamehe watuo hao waliofanya kitendo hicho kwa kuwa hawajui watendalo.


Katekista Edward Leiyan kutoka Parokia ya Nainokanoka, amesema kwa niaba ya wakazi wa Ngorongoro wanawaombea Msamaha waliofanya kosa hilo kwa kuwa Mungu hapendi Mikono inayomwaga damu, macho yenye kiburi, Ulimi wa Udanganyifu na Miguu inayokimbilia katika uovu.


Naye kiongozi wa mila Keswai Mepukori, amelaani vikali kitendo hicho na akisema hataki kitokee tena baada ya upatanisho walioufanya.


Viongozi hao wa kimila na Kiroho, wamechinja Ngombe watatu, mmoja kumwaga damu ishara ya kuomba radhi kwa uongozi wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro
Ng'ombe wa pili kwa ajili ya kuomba radhi kwa Serikali na waandishi wa habari kwa tukio lililotokea la kuwashambulia Waandishi wa habari ambao hawana hatia.


Ng'ombe wa tatu ni kwa ajili ya kumuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa tukio hilo huku akiwa na nia njema ya kuwafanya wananchi hao wawe na maisha mazuri katika maeneo salama yenye huduma stahiki.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...