Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Mamlaka
ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma PPRA imewasisitiza Wafanya biashara na
Wazabuni wote nchini Kuendelea kujisajili katika Mfumo mpya wa Ununuzi
wa Umma kwa njia ya mtandao NeST ili kuongeza ushindani na kupanua wigo
Mpana katika kuboresha uendeshaji wa Michakato ya ugawaji wa zabuni za
umma.
Akizungumza hayo Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA Bw. Eliakim
Maswi amesema kuwa, Idadi ya Wazabuni wanaojisajili kwenye Mfumo inazidi
kuongezeka siku hadi siku jambo linalotoa taswira Chanya juu ya
muitikio na mapokeo ya Wananchi katika ujio wa Mfumo huo mpya wa NeST
katika sekta ya Ununuzi wa Umma.
“Tunashkuru kupitia juhudi za
Serikali yetu Kuona idadi ya Wazabuni wanaojisajili ndani ya Mfumo
inaongezeka siku hadi siku suala ambalo hata sisi kama Mamlaka
tunalitazama kwenye mtazamo Chanya, Mpaka sasa Jumla ya Wazabuni 4,350
tayari wameshajisajili kwenye Mfumo” Alisema Maswi.
Sambamba na
suala hilo, Maswi amewataka Wazabuni Pamoja na Taasisi za Umma kuendelea
kushiriki mafunzo yanayoendelea kutolewa katika mikoa mbalimbali nchini
ambayo yanalenga kutoa muongozo wa namna ya matumizi sahihi ya Mfumo
huo wa NeST kwa Taasisi za Umma sambamba na Wazabuni wake.
“Utaratibu
wetu wa utoaji Mafunzo ya jinsi ya kutumia mfumo bado unaendelea,
Kwahivyo niwasihi Wazabuni Pamoja na Taasisi mbalimbali za Umma kuweza
kushiriki mafunzo hayo kwa mujibu wa ratiba zinazopangwa” Aliongezea
Aidha
amesema kuwa, Sambamba na Utoaji wa mafunzo hayo wanahakikisha kila
Taasisi inayopatiwa mafunzo inasajiliwa ndani ya Mfumo mpya wa NeST ili
mapema kuanza kutumia Mfumo huo bila kuwa na urasimu wa aina yoyote.
“Kila
Taasisi tunayoipatia mafunzo ya Mfumo mpya tunahakikisha tunaisajili
pia kwenye mfumo ili ikibidi waanze kutumia mfumo huu haraka” Alisema
Ifikapo
tarehe 30 Septemba Taasisi zote za Umma zinatakiwa ziwe tayari
zimeshajisajili kwenye Mfumo kwani Mpaka tarehe 1 Oktoba hakutakuwa na
Taasisi yoyote ya Umma itakayoweza kufanya michakato ya Ununuzi nje ya
mfumo wa NeST.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...