Agosti 14, 2023 Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) amezungumza na Vyombo vya Habari juu ya Utungwaji wa Sera ya Kampuni Changa za Ubunifu (Startups) katika Ofisi za Tanzania Startups Association (TSA), Jijini Dar es Salaam.
Katika Mazungumzo hayo Waziri Nape amesema kuwa msimamo wa Serikali wa kutungwa kwa Sera ya Kampuni Changa ni msimamo thabiti na utashirikisha wadau wa pande zote mpaka kukamilika kwake ili kuweza kuwa na Sera Bora ya kusimamia kampuni hizo.
“Serikali inakamilisha hatua za mwanzo za utungwaji wa sera ya Startups na itakapokamilika italetwa kwenu wadau kwa ajili ya kutoa maoni yenu.” Amesema Waziri Nape
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa TSA, Zahoro Muhaji amesema kutokuwepo kwa sera hiyo kunawazuia wao kuweza kufanya biashara na wanafurahishwa na hatua iliyochukuliwa na Serikali katika kukamilishwa kwake.
Pia, Waziri Nape amejionea na kuridhishwa na mazingira ya ofisi za Kampuni hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...