
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akikagua miundombinu ya uwanja wa kwaraa patakapo fanyika maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge wa uhuru 2023 Mkoani Manyara, kulia kwake ni Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar,Fatma Hamad Rajab.
Na. Mwandishi wetu Manyara
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema ameridhishwa na maandalizi ya shughuli za kilele cha mbio za mwenge wa uhuru 2023 Mkoani Manyara.
Prof. Ndalichako amesema hayo Mkoani humo alipofanya ziara kwa ajili ya kukagua maendeleo ya shughuli za kilele hicho zitakazofanyika Oktoba 14, 2023.
Aidha ameutaka uongozi wa mkoa huo kukamilisha ujenzi wa uwanja wa kwaraa kabla ama ifikapo Septemba 30, 2023.
Amempongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha zaidi ya shilingi Milioni 600 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja huo na miundombinu nyingine.
Prof. Ndalichako ametoa wito kwa watanzania hususan mikoa ya Jirani kujitokeza kushiriki katika maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge wa uhuru ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha, amekagua uwanja wa kwaraa yatakapofanyika maadhimisho hayo, Kanisa la Parokia Mtakatifu itakapo fanyika ibada ya Baba wa Taifa, uwanja wa stendi ya zamani itakapo fanyika wiki ya vijana na kukagua maendeleo ya vijana wa halaiki.
Waziri Ndalichako katika ziara hiyo aliambatana na Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar,Fatma Hamad Rajab.
Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka 2023 zinaongozwa na kauli mbiu isemayo “Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa ustawi wa viumbe hai na Uchumi wa Taifa”.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (wa tatu kushoto) akikagua uwanja wa stendi ya zamani itakapo fanyika wiki ya vijana Mkoani Manyara.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (wa tatu kushoto) akikagua Kanisa la Parokia Mtakatifu itakapo fanyika ibada ya Baba wa Taifa Mkoani Manyara





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...