
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt.Tulia Ackson amempongeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako na Naibu Waziri wa Ofisi hiyo, Mhe. Patrobas Katambi kwa kushughulikia kwa karibu masuala ya wastaafu.
Dkt.Tulia ametoa pongezi hizo Agosti 29, 2023 bungeni baada ya Naibu Waziri Katambi kujibu maswali ya wabunge kuhusu masuala ya wastaafu.
Amesema “Naibu Waziri ameonesha utayari kama Mbunge ana changamoto apelekewe, mimi ni shahidi wanafanya kazi nzuri Waziri Ndalichako na Naibu Waziri Katambi, wanasikiliza hoja ukiwapelekea na wanafuatilia kuhakikisha mtumishi au mstaafu anasaidiwa.”
Amesema kuna umuhimu wa kuendelea kutoa elimu kuhusu hifadhi ya jamii huku akipongeza maboresho yanayoendelea kufanywa kwenye utoaji huduma kwa wastaafu.
Awali, Naibu Waziri Katambi amesema serikali imekuwa ikishughulikia masuala ya wastaafu kwa kuwasikiliza na kutatua changamoto zao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...