Na Said Mwishehe, Michuzi TV
UONGOZI wa Klabu ya timu ya soka ya Yanga maarufu kama Wananchi ya jijini Dar es Salaam imewaomba mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kununua tiketi mapema kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya timu ya Asas Djibhouti ili kuepuka kununua 'tiketi feki'
Katika mchezo wa awali kwa timu hizo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 , mchezo uliochezwa Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam na mchezo wa marudiano Yanga itakuwa mwenyeji baada ya mechi ya awali kuwa ugenini.
Akizungumza leo kuelekea mchezo huo wa marudiano utakaochezwa Jumamosi ya 26, 2023 katika uwanja huo wa Chamazi , Msemaji wa Klabu ya Yanga Ally Kamwe mbali ya kutaja viingilio ambavyo ni Sh.5000, Sh.20, 000 na Sh.30, 000 amesisitiza umuhimu wa Wananchi kukata tiketi mapema kuepuka usumbufu unaotokana na kuchelewa kukata tiketi mapema.
" Tunaomba Wananchi wanunue tiketi mapema kuepuka usumbufu lakini pia kujiepusha na kuuziwa tiketi feki ambazo nyingi zinauzwa pale uwanjani na watu wanunua kumbe ni feki, hivyo wanapotaka kuingia uwanjani zinagoma.Hivyo tunashauri tukate tiketi mapema, ingia kwenye page ya Yanga utaona tunaelekeza tiketi bei yake na inauzwa wapi, "amesema Kamwe
Akifafanua zaidi kuhusu malalamiko ya kununua tiketi feki, amesema katika kukabiliana na changamoto hiyo Klabu imekuwa inajenga uelewa , kwanza kufahamu bei ya tiketi na zinakopatikana.
" Sisi tunatimiza wajibu wetu na taasisi nyingine zitimize wajibu wao.Klabu ya Yanga inatangaza vituo na kwenda kununua tiketi na vyombo vya ulinzi na usalama wachukue hatua ya kukamata watu wanaouza tiketi pale uwanjani.
"Hata hivyo watu wanapigwa kwasababu tu wameshindwa kufuata taratibu.Turudi kwenye mstari kwa kutonunua tiketi kwa watu wa mchongo.Tiketi za mchongo zinauziwa pale uwanjani, hivyo wananchi wanunue tiketi mapema, " amesema.
Ameongeza hakuna tiketi inauzwa na N-Card halafu mtu akashindwa kuingia uwanjani huku akifafanua N-card hawawezi kutoa tiketi tofauti na uwanja.
"Wenye tiketi feki wanapitishwa lakini wenye tiketi halali hawapitishwi kirahisi, .Tudhibiti wenye titeki feki wasiuze pale uwanjani tutakuwa tumemaliza tatizo.H
"Hata hivyo tunawapongeza Jeshi la Polisi kwa kusimamia utaratibu, idadi ya watu inapotimia hawaruhusu wengine kuingia ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea."
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...