MTU mmoja amefariki dunia na wengine sita wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyohusisha magari mawili moja likiwa Lori la mizigo na basi la abiria aina ya
Tata.

Akizungumzia tukio hilo Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro Emmanuel Ochieng amesema chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa gari la mizigo (Lori) kwa kutozingatia alama na michoro ya usalama wa barabarani iliyokuwepo katika eneo hilo.

Amefafanua lori lilikuwa likitokea uelekeo wa Msamvu na kuelekea uelekeo wa Iringa na basi la abiria lililokuwa likitokea Ifakara likielekea katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Msamvu Morogoro na kwamba ajali hiyo imetokea barabara kuu ya Morogoro – Iringa Manispaa ya Morogoro.

Pia Kamanda Ochieng amesema anayesadikiwa kupoteza maisha katika ajali hiyo ni dereva wa lori na mwili wake umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na wengine sita ambao ni majeruhi walikuwa kwenye basi la abiria na hadi sasa wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...