*Kanisa likijihusisha na siasa litakuwa na ubinafsi wa kupendelea upande mmoja
*Latangaza mkutano kufanyika Dar
Na Chalila Kubuda ,Michuzi TV
Kanisa la Halisi la Mungu Baba limesema katika utoaji huduma ya kiroho haijihusishi na Siasa kwani kufanya hivyo Kanisa linaweza kuwa na ubinafsi kwa kupendelea chama.
Licha ya kuwa hawajihusishi waumini wake hawatambuani kwa vyama na kufanya waumini kuwa familia moja kwa kufuata masuala ya Ki-Mungu.
Hayo aliyasema jijini Dar es Salaam kiongozi wa Kanisa Halisi la Mungu Baba, Baba Halisi wakati wa kutangaza mkutano utaofanyika Mlimani City Septemba 10 jijini Dar es Salaam utaohudhuriwa na makundi mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali.
Baba Halisi amesema Tanzania inatajwa kuwa chanzo cha baraka kufuatia amani, utulivu na rasilimali za nchi kutokana na uwepo wa uongozi unaozingatia haki.
alisema inatakiwa Watanzania kujua jinsi nchi ya Tanzania ilivyobarikiwa na Mwenyezi Mungu kwa kuwa rasilimali za kutosha.
Halisi amesema Watanzania wajitambue na kubadilisha mienendo yao kwa kuhakikisha wanakuwa baraka kwa wengine kutokana na rasilimali zilizopo ambapo mataifa mengine hayana rasilimali hizo.
"Kwa kuwa Tanzania imebarikiwa, Watanzania wanapaswa kubadilisha mienendo yao kwa kuchangua namna bora ya kuishi ili kuendelea kuwa baraka kwa mataifa mengine," amesema
Halisi alisema kanisa hilo limekuwa likiishi kwa kuhimiza amani, upendo, kuzalisha haki ndio maana limeandaa mkutano wa kijamii na utahudhuriwa watu zaidi ya watu 1000 kutoka ndani na nje ya nchi watashiriki.
Alisema mkutano huo utabebwa na mada isemayo Tanzania ndiyo chanzo cha baraka kwa mataifa yote lengo ni kuwapa uelewa Watanzania kuzitambua rasilimali zilizopo.
"Kanisa hili ili kuhakikisha rasilimali zinalindwa ikiwepo amani, upendo na kuzalisha haki, tumekuwa na desturi ya kila siku saa 11 asubuhi kuwaombea viongozi waliopo madarakani wazidi kuongoza kwa haki,"alisema.
Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Halisi la Mungu Baba, Baba Halisi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mkutano waliouandaa, Jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...