Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
MWENYEKITI wa Baraza la 12 la Uongozi Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT), Profesa, Ulingeta Mbamba amesema baraza hilo chini kufanya kazi ya uongozi wake, litahakikisha linafanya kazi ya ziada kuhakikisha kiasi kikubwa kllichowekezwa na serikali kwenye miundombinu ya usafirishaji hakipotei bure.
Amesema Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye miundombinu ya usafirishaji, hivyo hata wao hawana budi kufanya kazi ya ziada katika kuhakikisha wanaunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali kwenye sekta ya usafirishaji.
Akizungumza katika hafla ya kuliaga baraza la uongozi la 11 na kukaribisha baraza jipya la uongozi la 12, leo Septemba 30,2023 chuoni hapo, Mbamba pia amelipongeza Baraza la 11 lililomaliza muda wake kwa kufanya kazi kubwa ambayo Maendeleo yakr yamekuwa yakizidi kuonekana kila siku
Aidha ameishukuru menejimenti ya Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) kwa kuendelea kufanya vizuri, hivyo baraza lipo kwaajili ya kusaidia na maendeleo yaweze kuonekana zaidi.
Naye, Mjumbe wa Baraza la 11 la Uongozi wa Chuo, Mhandisi Eliona Simbo, akiongea kwa niaba ya Wajumbe wa Baraza , amesema kwa kipindi walichokuwepo walipata ushirikiano mkubwa na menejimenti ya Chuo hivyo kufanya kuonekana kwa maendeleo chuoni hapo
"Haya maendeleo yanayoonekana, hatuna budi kuishukuru menejimenti ya Chuo kwa ushirikiano mkubwa walioutoa pindi tunapoingia kazini kwa mara ya kwanza hadi kufikia mwisho na kuchaguliwa kwa Baraza lingine". Amesema
Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT), Profesa Zacharia Mganilwa amesema uanzishwaji wa Kituo cha Mafunzo ya Usalama Barabarani ambacho kinafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika ni moja ya mafanikio yaliyopatikana katika Uongozi wa Baraza la 12.
" Kutokana na wingi wa matukio ya ajali barabarani, kituo hiki kimedhamiria kupunguza ajali za barabarani". Amesema Profesa Mganilwa.
Mjumbe wa Baraza la 11 la Uongozi wa Chuo, Mhandisi Eliona Simbo akizungumza katika hafla ya kuliaga Baraza la Uongozi la 11 lililomaliza muda wake, hafla ambayo imefanyika leo Septemba 30,2023 Jijini Dar es Salaam










Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...