Na.Khadija Seif,Michuziblog 

BARAZA  la Sanaa Taifa (BASATA) limeahadi  kumshika mkono muandaaji wa shindano la Bongo star search Madam Rita kuhakikisha mashindano hayo yanaendelea kila mwaka 

Akizungumza na Wanahabari  Katibu Mtendaji wa Baraza la SanaaTaifa(BASATA) Dkt.Kedmon Mapana amesema wamatambua mchango mkubwa unaofanywa na Jaji mkuu ambae pia ndio Muasisi mkuu wa shindano hilo kupitia Kampuni ya The  Benchmark production amekuwa akiiona fursa kwa vijana mbalimbali katika soko la Muziki na kuwapa nafasi ya kutumia platform ya Bss kunyanyua vipaji hivyo na baadae kubadilisha maisha yao.

Hata hivyo Mapana ametoa pongezi zaidi kwa Vijana wote wanaoikimbia fursa ya Bss na kuona ipo haja ya kushikwa mkono kwa ngazi ya chini hadi kufika mbali zaidi walipofikia wanamuziki wanaipeperusha bendera ya  Tanzania.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa The Benchmark Production Rita Paulsen maarufu 'Madam Rita' amesema  ni Msimu wa 14 tangu kuanzishwa kwa Bss na Kuna mengi yamefanyika huku Msemo wa Msimu huo ni Kipaji chako Mtaji wako.

"Kupitia Bongo star search Vijana wengi wamebadilisha maisha yao hivyo Msimu huu wa 14 kipaji cha kila kijana kiende kuwa mtaji ili kiweze kumuingizia pesa na kubadilisha zaidi maisha yake na ya Muziki wake kwa ujumla."

Hata hivyo amesema Kuna maombi mbalimbali yaliweza kuwafikia ili kuwepo kwa Mabadiliko ya msimu mpya ikiwemo Mashabiki wa mkoa wa  Kigoma kuomba zoezi la usahili kufanyika mkoani humo baada ya kipindi kirefu kutofanyika kwa usahili mkoani humo.

"Kigoma Kuna vipaji tunatambua mchango mkubwa unaofanywa na Peter Msechu ni moja ya zao la Bongo star search hivyo kwa mwaka huu 2023 tutakuwepo Mkoa wa Kigoma Septemba 28 hadi 29 ,2023 ukumbi wa Kidyama Beach. "


Aidha,Paulsen amesema amegundua kuwepo kwa changamoto ya usimamizi wa wasanii na kazi zao mara baada ya Kumalizika kwa shindano hilo ,hivyo Kuna  kampuni imejitokeza na ambayo itashirikiana nao utashirikiana katika kusimamia wasanii watakaoshinda.


Hata hivyo  amesema Wakazi wa Arusha utafanyika usahili oktoba 7,8 ,na Wakazi wa Mwanza usahili utafanyika Oktoba 14 na 15, Mkoa wa Mbeya Oktoba 21na 22 wakati wakazi wa Jijini Dar es Salaam  watashuhudia usahili ukifanyika Novemba 3,4 na 5 mapema mwezi Novemba mwaka huu 2023.


Nae Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa amesema ni wakati wakuendelea kuunga mkono vijana kwenye vipaji vyao hasa Sanaa ambapo kwa sasa kupitia sekta ya Sanaa inaongeza pato la taifa.

''Wateja walipie vifurushi vyao ili waweze kuona show hii isio na mpinzani watashuhudia maudhui mbalimbali kuanzia kwenye usahili,kambini hadi kufikia finalized yenyewe huku kwa mwaka huu ikiwa na sura mpya au ingizo jipya la jaji ambae ni Shilole.


Pia amesema Shindano hilo litakuwa likiruka mubashara st swahili ambapo mapema mwezi January 2024 wanatarajia kuhitimisha shindano hilo.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...