Na Mwandishi Wetu

Benki ya Exim imetangaza kuendeleza dhamira yake ya kutoa huduma za kibenki kwa ufanisi mkubwa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake ya kuimarisha ushirikishwaji wa kifedha nchini .

Akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam Jumanne jioni, Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim Shani Kinswaga alisema benki hiyo imejizatiti kutekeleza kikamilifu mikakati wake wa kupunguza pengo la watu ambao bado halijafikiwa na benki.

Kinswaga alisema benki yake itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza ukuaji wa sekta ya benki hapa nchini huku akisisitiza malengo ya benki hiyo ya kuinua maisha ya wateja wake kupitia upatikanaji wa huduma za kifedha bila vikwazo, kupitia matumizi ya suluhu za kidijitali na huduma zinazotengenezwa mahususi.


“Tunashukuru sana kwa nafasi hii ya kipekee ya kuonyesha huduma zetu mbalimbali za kibenki kwa Jeshi la Polisi. Kama benki, tutaendelea kuwa mstari wa mbele kusogeza huduma za benki karibu na watu hasa katika ngazi za chini,” Kinswaga.

Kinswaga aliongeza kuwa mwanzoni mwa mwaka huu, benki ya Exim iliboresha mfumo wake na kuweka miundombinu thabiti, hatua inayolenga kuimarisha utendaji wake na kuwapa wateja hali ya juu ya usalama, ufanisi na uvumbuzi.

"Hii inadhihirisha ari yetu katika kubadilika na kuwa zaidi ya taasisi ya benki. Kama benki, tumejitolea kuwekeza katika kuongeza uwezo li wa mifumo yetu ilikutoa huduma bora kwa wateja wetu na jamii inayotuzunguka," Kinswaga alisema.

Kinswaga alisema wakati benki hiyo ikiadhimisha miaka 26 ya kuwa zaidi ya benki mwaka huu, benki hiyo inajivunia na itaendelea kuwawezesha Watanzania kupitia upatikanaji wa huduma za kifedha na bidhaa za kibenki, zilizoundwa kulingana na mahitaji yao.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo wa Benki ya Exim Andrew Lyimo wakati wa hafla hiyo alisema benki hiyo itaendelea kutoa masuluhisho yanayomlenga mteja pamoja na kuboresha ubora wa huduma kwa wateja wake kupitia chaneli za kidijitali ilikuvutia wateja wengi zaidi.

Alisema benki hiyo ina masuluhisho na bidha mbalimbali na ya kipekee huku akitaka miongoni yake kuwa pamoja na ‘Mkopo wa Wafanyakazi, Mkopo wa Nyumba, Haba na Haba na akaunti ya Super Woman ambazo huja na manufaa zaidi kwa wateja watarajiwa.

Lyimo alisisitiza kuwa mkopo wa benki hiyo wa ‘Wafanyakazi’ ni maalumu kwa watumishi wa Serikali na unaweza kurejeshwa hadi miezi 96 na hauhitaji dhamana yoyote kwa wakopaji wanaostahili huku akiongeza kuwa mkopaji anauwezo wa kukopa kima cha chini cha shilingi milioni moja na kiwango cha juu hadi shilingi milioni 160.

"Sisi kama Benki ya Exim tumekuwa na shauku ya kutengeneza fursa kwa wateja wetu kwa kutoa huduma zinazoongeza thamani sambamba na kutoa huduma bora kwa wateja wetu. Nachukua fursa hii kuwaomba Watanzania wote kuchangamkia fursa hizi zinazotolewa na benki yetu ya Exim ili nao waendele kunufuaika,” Lyimo alisema.

Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim Shani Kinswaga (kushoto) akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam Jumanne jioni uliongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Camilius Wambura. Benki hiyo iliwataka maafisa wakuu wa polisi kuchangamkia fursa zinazotolewa na benki hiyo. Picha na Mpiga Picha wetu

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo wa Benki ya Exim Andrew Lyimo akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam Jumanne jioni uliongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Camilius Wambura. Benki hiyo iliwataka maafisa wakuu wa polisi kuchangamkia fursa zinazotolewa na benki hiyo. Picha na Mpiga Picha wetu
Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim Shani Kinswaga (kushoto) akizungumza na Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Pilisi ACP Anthony Ruta (wa tatu kushoto) mara baada ya Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania uliofanyika jijini Dar es Salaam Jumanne jioni uliongozwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Camilius Wambura. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo wa Benki ya Exim Andrew Lyimo. Benki hiyo iliwataka maafisa wakuu wa polisi kuchangamkia fursa zinazotolewa na benki hiyo. Picha na Mpiga Picha wetu .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...