Na Mary Margwe, Geita
Naibu Waziri Mkuu na Waziri Mkuu wa Nishati Dotto Mashaka Biteko anatarajia kuwa Mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Maonyesho ya sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini yatakayofunguliwa Septemba 23 Mwaka huu katika Halmashauri ya Mji wa Geita huku Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan akitarajiwa kufunga Maonyesho hayo.
Hayo yamebainishwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigelawakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya EPZA vilivyopo katika Kata ya Bombambili Halmashauri ya Mji wa Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigela amesema,maonyesho ya mwaka huu yamekuwa na mwitikio mkubwa kutoka na kuwepo Kwa washiriki wengi zaidi kujitokeza kuonyesha shughuli wanazozifanya ukilinganisha na Mwaka Jana.
Shigela amesema Mwaka 2018 Mkoa wa Geita ulianzisha Maonyesho ya Teknolojia ya Madini dhamira ikiwa ni wananchi kupata maarifa mapya watakayoyatumia katika shughuli ya uchimbaji wa madini, utafiti, uongezaji thamani, na uchechuaji.
“ Maonyesho haya yalianza 2018 na mwaka huu ni maonyesho ya sita ya madini ambapo dhamira ni kuhakikisha kwamba wananchi wanapata maarifa mapya watakayoyatumia katika shughuli za utafiti,kuongeza thamani na shughuli za uchenjuaji,
Aidha amefafanua kuwa mwaka jana walipata washiriki 250 ukilinganisha na Mwaka huu washiriki walioimgia ni zaidi ya 400, ambapo amesema hiyo ni kutokana na mwitikio mkubwa wa wanachi wachimbaji, Wafanyabiasha hasa makampuni yanayojihusisha na utafiti wa Madini, yanayojihusisha na uchechuaji, yanayojihusisha na Uchimbaji, yanayojihusisha na Teknolojia ya uongezaji thamani.
Shigela amesema hiyo yote inatokana na kuwepo Kwa uelewa wa maana Maonyesho, kwani wameona umuhimu wa kuja kwenye hayo Maonyesho, hivyo ninvema wananchi hususani wananchi wajimbaji wakajitokeza Kwa wingi ili kuja kujifunza Teknolojia nanmaarifa mapya yatakayoyatoa hapo walipo na kuwapeleka kwenye viwango vingine.
" Mwaka huu washiriki walioingia mpaka sasa ni zaidi ya 400 maana yake mwitikio ni mkubwa na wananchi hasa wachimbaji wameelewa maana ya uchimbaji hususan makampuni yanayojihusisha na uchimbaji,uchenjuaji ,uongezaji thamani kwa maana kwamba wameona umuhimu wa kushiriki katika maonyesho haya.”amesema Shigela
Aidha amesema Mkoa umeweka mazingira mazuri ili kuwawezesha wadau wa sekta ya madini kuja na teknlojia mpya na rahisi zitakazowawezesha wachimbaji wadogo kufaidika na teknolojia hizo kwa gharama ndogo za uchijimbaji ,uchenjuaji na uongezaji thamani wa madini ili nchi ifikie hatua ya kuhifadhi dhahabu ambayo imeongezwa thamani kwa zaidi ya asilimia 100.
" Sisis kama Mkoa tumeshaweka Mazingira mazuri ya kwanza ya kuwapokea makampuni yote yanayojihusisha na utafitiwa Madini ili wake na Teknolojia mpya lakini Teknolojia rahisi itakayowawezesha wachimbaji wetu wadogo kufaidika na hiyo Teknolojia" amesema Shigela.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa Shigela pia ametuamia nafasi hiyo kuwakaribisha wananchi hasa wanaojishughulisha na uchimbaji,uongezaji thamani na uchenjuaji wa madini kufika katika viwanja hivyo kujifunza na kujionesha mitambo na mshine kwa ajili ya shugfhuli za uchimbaji.
.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...