Na Nasara Ismail, Geita

Elimu na uelewa mdogo kuhusu urasimishaji wa biashara imekuwa changamoto kubwa kwa wafanyabiashara hali iliyowasukuma wakala wa leseni na biashara BRELA kuweka banda katika maonesho ya 6 ya teknolojia ya madini ili kutoa elimu hiyo.

Hayo yamesemwa na kaimu mkurugenzi wa kurugenzi ya miliki ubunifu kutoka wakala wa usajiri wa biashara na leseni BRELA Roi Mhando wakati akiongea na waandishi wa habari wa mkoa wa Geita katika maonesho ya madini yanayotajaiwa kufunguliwa rasmi mnamo June 23.

Roi aliwasihi wafanyabiashara kufika mapema katika banda la brela ili kujipatia elimu bure na kufanya usajiri wa papo hapo ili kila mfanyabiashara aweye kuwa katika mfumo rasmi.

“jukumu letu sisi hapa ni kutoa elimu kwa wadau wote na kama mnavyofahamu BRELA ndio mlango wa urasimishaji wa biashara nchini ambapo mdau muwekezaji au mfanyabiasha anaanza kwanza kurasimisha biashara yake ndipo anaendelea katika hatua nyingine” Alisema Roi.

Aidha Roi aliongeza kuwa wamepokea maelekezo kutoka kwa naibu waziri wa viwanda na biashara mh Exaud Kigahe ya kuhakikisha wanawawezesha wafanyabiashara badala ya kuwa kikwazo kwao katika utoaji wa huduma. 

“tunatoa huduma zetu zote kwa njia ya mtandao kwahiyo mdau popote alipo mradi tu aweze kupata vifaa vya kuingia kwenye mtandao sio lazima azifate ofisi zetu zilipo” Alisema Roi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...