NA WILLIUM PAUL, KILIMANJARO.

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka mshindi katika uchaguzi mdogo wa marudio ya Udiwani katika kata za Old Moshi magharibi wilayani Moshi na Marangu kitowo wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.

Uchaguzi huo uliofanyika jana ambapo katika kata ya Old Moshi magharibi kulikuwa na wagombea wa vyama saba ambao ni Peter Massawe (CCM) aliyepata kura 3538.

Wagombea wengi na idadi ya kura walizopata ni Florence Saria (SAU) kura 38, Stephen Machange (NCCR Mageuzi) kura 81, Edward Mosha (ADC) kura 23, Luckresia Mkenda (ADA-TADEA) kura 11, Elisaria Macha (DP) kura 13, na Samweli Owenya (NRA) kura 14.

Katika kata ya Marangu kitowo wilayani Rombo kulikuwa na wagombea watano ambapo mgombea wa Chama cha Mapinduzi Simon Massawe aliibuka mshindi kwa kupata kura 1659.

Wagombea wengi kata kata hiyo ni Dionis Shirima (SAU) alipata kura 101, August Baimu (ADA -TADEA) kura 12, Nestory Kimario (DP) kura 15, na Clemence Kimario (TLP) kura 6.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...