Na Nasra Ismail, Geita

Takribani Mataifa 6 yanatarajia kushiriki katika maonesho ya madini ambayo yalizinduliwa mnamo septemba 20 ambayo yanafanyika katika viwanja vya EPZA katika mtaa wa bomba mbili katika mkoa wa Geita  huku yakitarajiwa kufungwa na mh Raisi Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela aliyataja mataifa hayo kuwa ni Rwanda,Burundi,Kenya,China, Malawi pamoja na DRC Congo.

Shigela aliwakaribisha mataifa mengine kuja kwa wingi  kwenye maonesho haya ili  kujifunza namna teknolojia mpya ya uchimbaji inavyofanyika.Aidha Shigela aliongeza kuwa hamasa kubwa inayofanyika katika maonesho haya inasukuma maendeleo makubwa kwa serikali na wafanyabiashara katika mkoa wa Geita kutokana na faida kubwa wazoingiza kupitia maonesho haya.

“wananchi wa geita wakisikia maonesho haya yamefutwa huyo kiongozi aliyeshiriki kuyafuta atalaaniwa milele na wananchi ,ukiacha serikali kupata fursa ya kimapato lakini wafanyabiashara wa mkoa wa Geita wanapata faida kubwa sana, leo ukienda kwenye mahoteli hakuna chumba utakipata kwasababu hamasa ya ushiriki ni kubwa sana” alisema Shigela.

Kwa upande mwingine Shegeka aliwatoa hofu washiriki wanaotamani kushiriki katika maosneso hayo kuwa mkoa ni salama na wanaotamani kushiriki waje kwa wingi na teknolojia mpya na raisi ili kuwasaidia wachimbaji wadogo kuweya kuitumia technolojia hiyo.

“Sisi kama mkoa tumeshaweka mazingira mazuri ya kuwapokea makampuni yote yanayojihusisha  na uchimbaji na utafiti wa madini kuja na teknolojia rahisi ili ya kumuwezesha mchimbaji mdogo kwa gharama ndogo ili aweye kumudu.” Alisema Shigela.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...